Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Shahid Khamenei (ra) mwanzoni mwa vikao vya darsa yake ya Bahthul-Kharij ya Fiqhi, alikuwa akifafanua Hadithi ya kimaadili, “Kuamiliana kwa upole na watu” ni mada ya ufafanuzi wa Hadithi ya kimaadili kutoka kwa Mtume mtukufu wa Uislamu, Mtume Muhammad (saww), ambayo vmatini yake imechapishwa hapa chini, matini ya maelezo ya Kiongozi Shahid ni kama ifuatavyo:
Bismillahir-Rahmanir-Rahim
Alhamdulillahi Rabbil-'Alamin
Kutoka kwa Mtume (saww) ni mwendelezo wa Hadithi ambayo hapo kabla baadhi ya vipande vyake vilielezwa:
«أعقل الناس أشدهم مداراتاً للناس»
Mwenye akili zaidi kwa watu, ni yule ambae anaamiliana zaidi na watu kwa upole.
“Mudaraat” maana yake ni kuamiliana vizuri na watu.
Maana yake ni hii: Kufanya mudara ni kuafikiana, kutotafuta sehemu za mivutano na hitilafu, hii ndiyo maana ya mudara.
Wakati mwingine mwanadamu ana mgogoro wa msingi na mtu fulani, kuna haki na batili kati yao; hilo ni jambo jingine, lakini ikiwa hali si hivyo, inawezekana kuafikiana na upande mwingine; iwe katika biashara, katika mahusiano ya kisiasa, katika mahusiano ya kijamii au katika familia. Anasema: Mwenye akili zaidi miongoni mwa watu ni yule anayewafanyia wengine mudara zaidi kuliko wote, sababu yake pia iko wazi.
Kwa sababu mudara katika jamii huandaa utulivu na maisha mepesi kwa wote, kinyume na wale ambao daima wanataka kuwakwamisha wengine, unawakuta kwa kila jambo, kwa kila nukta ndogo tu, wanakuwa wakali, wanaudhi na kubishana; hili ndilo hasa lililo kinyume na mudara. «وأولى الناس بالتهمة من جالس أهل التهمة» Na mtu aliye karibu zaidi na kustahiki kutuhumiwa ni yule anayekaa na watu wanaotuhumiwa.
Haya pia ni maelekezo ya kiakili na ya kimantiki, anasema kwamba miongoni mwa watu wote, aliye tayari zaidi na anayestahiki zaidi kutuhumiwa ni yule anayekaa na watu wenye tuhuma, ndivyo ilivyo.
Amesema: «اتقوا مواضع التهم» Jiepusheni na sehemu za tuhuma.
Wote wanapaswa kuzingatia jambo hili, kukaa na kushirikiana na mtu anayeshutumiwa kwa jambo fulani, kwa kosa fulani au kwa ufisadi fulani, kunapelekea mwanadamu kuelekezewa tuhuma.
«وأعتى الناس من قتل غير قاتله أو ضرب غير ضاربه»
Na dhalimu zaidi miongoni mwa watu, mkiukaji zaidi na mwenye jeuri zaidi ni yule anayemuua mtu ambaye hakuwa na nia ya kumuua yeye; au anayempiga mtu ambaye hampigi yeye.
Maoni yako