Jumanne 12 Mei 2026 - 17:30
Mwakilishi wa Ayatollah Sayyid Ali al-Sistani katika Haram ya Imam Hussein amesisitiza/ Uhusiano wa karibu zaidi baina ya Hawza ya Iran na Iraq

Hawza/ Sheikh Abdulrazzaq amesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarishwa zaidi kwa ushirikiano kati ya Hawza ya Iran na Hawza ya Iraq.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Kashan Iran, Sheikh Abdulrazzaq, mwakilishi wa Ayatollah Sistani katika Haram ya Imam Hussein (a.s), pembeni mwa hafla ya kupandishwa bendera ya Jamhuri ya Kiislamu katika uwanja wa kuingilia wa Ataba Tukufu ya Ali ibn Imam Muhammad al-Baqir huko Mashhad Ardehal, Kashan, na katika mkutano wake na mkurugenzi mtendaji wa Ataba hiyo tukufu pamoja na kundi la viongozi mbalimbali, huku akimshukuru meya maalumu wa wilaya ya Kashan, alisema katika majibu yake kwa mwandishi wa shirika la habari la Hawza kwamba: Kashan, kutokana na kuwa na watu wenye taqwa, wanazuoni mashuhuri na historia ya kale, ni mji wa waumini.

Mwakilishi wa Marji' huyo katika Haram ya Imam Hussein (a.s), huku akibainisha kwamba baada ya kuelekea nchini Iraq atawafikishia watu wa nchi hiyo, hususan jamaa na ndugu zake, ukarimu na mapokezi mazuri ya watu wa Kashan, alisema: Ziara yangu katika viwanda vya uzalishaji wa bidhaa za viwandani, bustani za maua ya waridi, pamoja na maziara ya watoto wa Maimamu katika eneo la Kashan, ilikuwa ya kuvutia sana na ya kushangaza.

Sheikh Abdulrazzaq, huku akirejelea ushirikiano uliopo baina ya Hawza za elimu za Iraq na Hawza za elimu za Qum na Kashan, alisisitiza juu ya umuhimu wa kuongezwa zaidi kwa ushirikiano kati ya Hawza za elimu za Iran na Hawza za elimu za Iraq, na akasema: Watu wa Iran na Iraq, kama Umma mmoja, wapo pamoja chini ya bendera ya Imam Hussein (a.s).

Aliongeza kusema: Iran ndiyo nchi pekee ambayo watu wa Iraq wana mapenzi na mshikamano wa pekee nayo. Aidha, Morteza Valizadeh, mshauri wa meya na mkurugenzi wa Shirika la Utamaduni, Jamii na Michezo la Kashan, naye huku akirejelea shakhsia tukufu ya Ali ibn Muhammad al-Baqir, mtoto wa moja kwa moja wa mtukufu Imam Muhammad al-Baqir, alisema: Ali ibn Muhammad al-Baqir akiwa balozi wa kwanza wa Wilayah nchini Iran, alitumia miaka mitatu kamili katika eneo la Kashan na maeneo ya jirani akisimamisha Swala za Jamaa, kufundisha maarifa safi ya Kiislamu, kubainisha hukumu za dini, na kueneza utamaduni halisi wa Kishia.

Mkurugenzi wa Shirika la Utamaduni, Jamii na Michezo la Manispaa ya Kashan pia katika hafla hiyo alisema kwamba; Mkoa wa Kashan mwaka uliopita ulichaguliwa kuwa mji wa nne wa hija nchini Iran, alisema: Baada ya Mashhad kutokana na kuwepo kwa Haram ya Imam Reza, Qom kutokana na Haram ya Fatimah al-Ma'sumah, na Shiraz kutokana na Haram ya Shah Cheragh, Kashan pia kutokana na Haram ya Ali bin Imam Muhammad al-Baqir (a.s) huko Mashhad Ardehal, ilichaguliwa kuwa mji wa nne wa hija nchini.

Mahdi Nadali, mjumbe wa Baraza la Kiislamu la Jiji la Kashan, pia akitangaza utayari wa mji huo kuwapokea mazuwari wa Iraq kwa mfumo wa misafara, alisema: Uongozi wa jiji la Kashan pamoja na Ataba Tukufu ya Ali bin Imam Muhammad al-Baqir (a.s) uko tayari kuwahudumia watu wa Iraq.

Pia, Meysam Namaki, mkuu wa Idara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya wilaya ya Kashan, alimtaja Mohtasham Kashani kuwa ni mtungaji mkubwa wa mashairi ya maombolezo katika ulimwengu wa Kiislamu, na akasema: Mohtasham Kashani ndiye mtungaji mkubwa zaidi wa mashairi ya maombolezo ambaye alitunga “Tarkib-Band” ya Imam Hussein (a.s), na mashairi hayo yametumika kama maandishi ya vibao vya maombolezo katika Husseiniyya za Iran na nje ya Iran, yakitumiwa na watu mbalimbali duniani hususan wanaozungumza Kiajemi.

Mkuu wa Idara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya wilaya ya Kashan alisisitiza: Tunatarajia kufanyika kwa usiku wa mashairi kwa jina la Imam Hussein (a.s) na Abu al-Fadl al-Abbas kwa lugha mbili za Kiarabu na Kiajemi, chini ya uenyeji wa Kashan na baadaye nchini Iraq katika Ataba Takatifu, kwa ushiriki wa washairi mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha