Jumanne 28 Aprili 2026 - 10:50
Mapinduzi ya Kiislamu daima yamesimama dhidi ya ubeberu wa Marekani na Israel

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika hotuba yake alisema: ikiwa duniani kuna yeyote aliyesimama dhidi ya ubeberu wa Marekani na Israel na kuupinga kwa mapambano, basi ni Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran; kwa hiyo, uadui mkuu pia umeelekezwa dhidi ya roho na ujumbe wa mapinduzi haya.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika hotuba yake alisema: lengo kuu la kumuua shahidi kiongozi, Ayatullah al-‘Udhma Sayyid Ali Khamenei, kiongozi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa hakika lilikuwa ni kuyakomesha Mapinduzi ya Kiislamu; kwa sababu mapinduzi haya ndiyo harakati ambayo katika miaka yote hii imekuwa ikipinga mfumo wa ubeberu, ukoloni, utumwa, dhulma, ukosefu wa haki na mfumo wa kitabaka unaoitawala dunia. Na ikiwa duniani kuna yeyote aliyesimama dhidi ya ubeberu wa Marekani na Israel na kuupinga, basi ni Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran; kwa hiyo, uadui mkuu pia umeelekezwa dhidi ya roho na ujumbe wa mapinduzi haya.

Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan aliongeza kusema: maadui kwa kumuua shahidi Ayatollah al-‘Udhma Sayyid Ali Khamenei walijaribu kuondoa roho ya mapinduzi; kwa hiyo, kuhuisha roho hii na kulinda ujumbe wa mapinduzi ni wajibu wa sote.

Aliendelea kusema: masuala kama uhuru, kujitegemea, kuikomboa Quds na kutetea haki za watu wa Palestina ni miongoni mwa mambo ambayo Mapinduzi ya Kiislamu yameyafanya kuwa ya wazi katika ngazi ya kimataifa. Kabla ya mapinduzi, wengi hata hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu haki za Wapalestina na kukaliwa Quds, ilhali leo ni wajibu wa kila mmoja kuinua sauti kwa ajili ya kuikomboa.

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Kipakistani pia alisema kuwa, ana ufahamu kamili wa hali ya ndani ya Pakistan, na kwa hekima na busara, hatua zimechukuliwa ili kuongoza sera za nchi katika mwelekeo sahihi. Na leo Pakistan, katika mtazamo wa Iran na Mapinduzi ya Kiislamu, inahesabiwa kuwa ni nchi inayoweza kuaminika, na katika njia hii juhudi zao pia zimekuwa na mchango.

Aliendelea katika hotuba yake kwa kuashiria juhudi za kuunda mazingira ya umoja na mshikamano nchini na kusema: daima hatua za vitendo zimechukuliwa kwa ajili ya kuimarisha mshikamano.

Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, pia alibainisha kuwa; fatwa ya kiongozi shahidi kuhusu kujiepusha na kuvitukana vitakatifu na kusisitiza umoja imekuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha mshikamano huu.

Aliongeza kusema: mwenendo wa madhehebu, uundaji wa makundi na uhamasishaji wa kijeshi ulioanza nchini, kwa hakika ilikuwa ni juhudi za kudhoofisha uungaji mkono wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Mwishoni, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi alisisitiza umuhimu wa kuimarisha umoja, mshikamano, uvumilivu, subira na ustahimilivu pamoja na harakati za pamoja miongoni mwa safu za wananchi, na akasema: hii ndiyo roho ya mapinduzi.

Pia alitoa nasaha ya kujiepusha na tabia hasi na kuwazuia walio karibu na mtu dhidi ya mienendo kama hiyo ili mazingira bora na yenye kujenga yaweze kuundwa katika jamii na taifa liweze kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha