Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad Qabalan alisisitiza kwamba; muqawama, jeshi la Lebanon, amani ya ndani, kulinda mamlaka na ushiriki wa kitaifa ni msingi mkuu wa nchi hii.
Katika tamko lake alisema: Inasikitisha kwamba; badala ya kuthamini kujitolea kwa kitaifa kulikofanywa na watu wa Kusini, Dhahiya, Bekaa na Beirut katika miongo kadhaa, baadhi ya maafisa ambao wamevutiwa na nafasi za utekelezaji wa ajenda za wengine bila kujali, wamechukua hatua ya aibu ya kupiga picha na muuaji wa Kizayuni huko Washington; kwa sababu kile kinachotokea nchini katika ngazi ya baadhi ya viongozi wa kisheria ni fedheha na tangazo la wazi la uadui dhidi ya watu wa nchi hii kwa namna ya kushtua. Hivyo nasema: Lebanon haiwezi kuvumilia kuwepo kwa “Napoleon mpya”, na kila kamari katika mwelekeo huu itapata hatima sawa na ya Napoleon.
Sheikh Qabalan aliongeza: “Israel”, ambayo ilimeza majeshi ya Waarabu kwa muda mfupi, safari hii imekabiliwa na muqawama katika mipaka ya mwanzo na imezuiliwa nayo. Propaganda za kile kinachoitwa “eneo la njano” hazina thamani yoyote, kwa sababu muqawama sasa uko katika maeneo ya al-Khiyam, Bint Jbeil, Aitata, al-Tayba, Shama, al-Bayada na al-Jbeen. Kuuawa kwa wanajeshi wa jeshi la Kizayuni katika eneo la al-Jbeen siku ya jana ni ushahidi wa wazi kwamba propaganda za “eneo la njano” si chochote isipokuwa ni dhana ya kufikirika inayokaa katika mawazo ya Netanyahu, mchinjaji aliyeshindwa.
Aliendelea kusema: Kwa wale wanaojali jambo hili, nasema kwamba Lebanon ni nchi yenye itikadi ya kitaifa na ina mistari myekundu ya kitaifa isiyoweza kuvukwa, na kuivuka ni hatari kubwa. Kutegemea kwamba watoto wa nchi hii watapigana na watoto wa muqawama wa kitaifa ni jambo hatari, bali ni janga, na kila mpango wa aina hiyo hautakuwa na hatima isipokuwa kushindwa.
Mwanachuoni huyo wa Kishia wa Lebanon alisema: Lebanon bila muqawama ni zaidi ya shamba lililogawanywa, linaloishi kwa utegemezi na kushindwa hata katika fikra, hisia, nafasi na wajibu wake. Enzi ya udhaifu au kuuza Lebanon na utambulisho wake wa kitaifa imekwisha muda mrefu uliopita. Kila taasisi ya kitaifa hubaki tu pale inapotekeleza wajibu wake wa kitaifa, na inapoupoteza wajibu huo, basi huangamia. Uzoefu wa Lebanon katika hili unajulikana, lakini baadhi wanapaswa kuelewa kwamba kuilinda Lebanon na uamuzi wake wa kitaifa ni wajibu wa mamlaka na taifa; na ikiwa Lebanon itageuka kuwa ya Kizayuni, haitakuwa na thamani yoyote.
Aliongeza kuwa: Jeshi la Lebanon limekuwa, na litaendelea kuwa taasisi ya kitaifa na ya mamlaka. Tishio lolote linalolenga uhalali, itikadi na jukumu la mamlaka la jeshi la Lebanon litalalizimisha taifa lote la Lebanon kusimama pamoja na jeshi hilo dhidi ya wasaliti wa Lebanon, taasisi zake za kitaifa na itikadi yake ya kihistoria. Mchezo wa nguvu za kisiasa uko wazi na fedheha imefunika sura yake. Kuvuka mistari myekundu kunaiweka Lebanon katikati ya janga ambalo haiwezekani kulinyamazia.
Sheikh Ahmad Qabalan alisema: Kinachotakiwa kwa baadhi ni kusoma historia ya Lebanon kwa umakini, kwani wazimu wa kujikweza kupita kiasi ni ugonjwa hatari, na haiwezekani kumwamini mwenye tabia hiyo wala kunyamazia maamuzi yake ya kipumbavu. Lebanon kwa asili yake imejengwa juu ya kuishi pamoja, amani ya ndani, ushiriki wa kitaifa na maadili. Lau si mchezo wa kulaaniwa wa ukoloni wa Ufaransa kuhusu ubaguzi wa kimadhehebu, leo Lebanon ingekuwa mfano mkubwa wa uadilifu, ushiriki na nguvu ya kitaifa ambayo ingezuia kugeuzwa kafara kwa maslahi ya baadhi ya wanaocheza kamari ya kisiasa.
Alisisitiza kuwa: Muqawama, jeshi la Lebanon, amani ya ndani, kulinda mamlaka ya taifa na ushiriki wa kitaifa ni mambo ya msingi yasiyoweza kuepukika kwa nchi hii, na hakuna yeyote anayeweza kuyavuka. Na yeyote atakayevuka mipaka hiyo, amejitia katika maangamizi, lakini hataweza kuiangamiza Lebanon.
Maoni yako