Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ra‘d al-Bahili, mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu na Kitamaduni cha Basra, Iraq, katika kongamano la kimataifa la Arubaini ya shahada ya Imamu Khamenei, lililofanyika jana jioni kwa ushiriki wa wanafunzi wa hawza na wanafunzi wa vyuo kutoka ulimwengu wa Kiislamu katika ukumbi wa Shahid Avini mjini Qum, alisema: Leo vita kati ya Iran na ubeberu wa kimataifa unaoongozwa na Marekani na Israel mhalifu, ni vita kati ya haki na batili.
Aliongeza: Leo katika upande wa haki wapo wapenda uhuru, watetezi wa uadilifu, waungaji mkono wa ubinadamu na watu wenye heshima; na upande wa pili wapo madhalimu, wakandamizaji, wauaji na wahalifu.
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema: Ujumbe wetu kwa Maimamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kwamba bendera iliyokuwa mikononi mwenu hadi jana, leo iko mikononi mwa kiongozi faqihi, shujaa na wa wananchi mwenye utambuzi na uelewa, ambaye hata siku hamsini baada ya shahada ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu bado yuko katika uwanja wa mapambano.
Umoja na mshikamano wa mhimili wa muqawama wa Kiislamu
Sheikh Ra‘d al-Bahili, huku akisisitiza tena uungaji mkono wa wapenda uhuru dunianj kwa upande wa haki, alisema: Leo si tu mhimili wa muqawama wa Kiislamu, bali watu wote huru duniani waungaji mkono na watetezi wa upande wa haki na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mhadhiri huyu wa hawza ya Iraq aliendelea kusema: Leo mhimili wa muqawama wa Kiislamu huko Lebanon, Palestina, Yemen na Iraq uko katika hali ya utayari kamili, na iwapo kutatokea ujasiri wowote wa maadui, watatoa funzo la kuzingatiwa kwao. Uwanja wa muqawama katika eneo lote umeratibiwa, na mhimili wa muqawama wa Kiislamu uko tayari kwa umoja na mshikamano kupambana na maadui.
Maadui wajue mhimili wa muqawama unaiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Mwanaharakati huyu wa kitamaduni wa Iraq aliendelea kusema: Ni kweli kwamba ulimwengu wa Kiislamu umepoteza shakhsia yenye athari kubwa na ya kipekee pamoja na kiongozi shujaa na wa wananchi, lakini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na uangalizi wa Imamu wa Zama (ajtf)، bendera hii imekabidhiwa kwa kiongozi mwenye elimu na uadilifu, na Inshaallah bendera hii kupitia kwake itamfikia Imamu wa Zama (ajtf).
Mwisho, Sheikh Ra‘d al-Bahili alisema: Maadui wajue kwamba leo mhimili wa muqawama wa Kiislamu ni msaidizi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na watu wote huru duniani na eneo hili pia ni waungaji mkono wa nchi hii ya Imamu wa Zama (ajtf). Wamarekani, Waisraeli na mawakala wao wote wajue kwamba mwisho wa kupigana na upande wa haki na ukweli ni maangamizi yao.
Maoni yako