Jumanne 14 Aprili 2026 - 12:30
Kwa nini Radi Amali ya Iran Dhidi ya Uvamizi Yalaaniwa, Lakini Jinai ya Mvamizi Inapuuziwa?

Hawza/ Wanazuoni wa Ahl al-Sunnah nchini Iran, katika barua ya wazi kwa Katibu Mkuu wa Muungano wa Umoja wa Kiislamu, wamesisitiza juu ya kutokuwa sahihi kwa baadhi ya taarifa za hivi karibuni za taasisi hiyo katika kulaani mwitikio wa Iran dhidi ya uvamizi wa Marekani kutoka katika nchi za ukanda wa Ghuba ya Uajemi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, wanazuoni wa Ahl al-Sunnah wa Iran katika barua ya wazi kwa Sheikh Dkt. Muhammad bin Abdul Karim al-Issa, Katibu Mkuu wa Muungano wa Umoja wa Kiislamu, huku wakikosoa baadhi ya taarifa za hivi karibuni za taasisi hiyo—ambazo kwa mtazamo wao hazikuwa na usahihi na uadilifu unaotakiwa—wamesisitiza haki halali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kujilinda, na wametaka kufanyiwa marekebisho misimamo inayochochea mgawanyiko pamoja na kuwaunga mkono wanyonge katika ulimwengu wa Kiislamu.

Matini kamili ya barua hii, ambayo inasisitiza umuhimu wa kutozipuuza jinai za maadui wa Umma na kuimarisha safu ya ndani ya ulimwengu wa Kiislamu, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kwa Mheshimiwa Sheikh Dkt. Muhammad bin Abdul Karim al-Issa, Katibu Mkuu wa Rabitat al-‘Alam al-Islami, Mwenyezi Mungu amlinde

Amani iwe juu yenu na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu

Sisi wanazuoni wa Ahl al-Sunnah wa Iran, kwa heshima na taadhima kubwa kwenu, tunathamini sana juhudi za "Muungano wa Umoja wa Kiislamu" katika kuhudumia masuala ya Umma wa Kiislamu. Pia tuna imani na hadhi yenu kubwa ya kielimu na fikra zenu angavu, kwa kuwa nyinyi ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa na wanafikra mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu.

Sisi tunaamini kuwa Saudi Arabia na Iran ni mabawa mawili katika ulimwengu wa Kiislamu, na kuimarisha uhusiano wa kindugu na ushirikiano baina yao ni kwa manufaa ya Umma wote wa Kiislamu. Sisi daima tunalenga kuimarisha mawasiliano na mazungumzo yenye kujenga ambayo yanakaribisha mitazamo.

Katika muktadha huo, kwa masikitiko, tunalaani baadhi ya taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na Rabitat al-‘Alam al-Islami; taarifa ambazo zilijumuisha tuhuma ambazo kwa mtazamo wetu hazikuwa sahihi wala za haki. Kauli hizi zimetolewa katika wakati ambao Umma unahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote umoja na mshikamano katika kukabiliana na changamoto kubwa.

Mapambano halisi ambayo Umma wetu unakabiliana nayo ni mapambano ya Uislamu dhidi ya nguvu za ukafiri na ubeberu, zinazoongozwa na mhimili wa Marekani na Uzayuni. Katika hali kama hii, kuchapisha taarifa zinazokosoa mwitikio wa kujilinda ulio halali, huku zikifumbia macho jinai kubwa zinazofanywa dhidi ya Waislamu—ikiwa ni pamoja na mauaji ya watu wa dini na wasomi na kulenga shule na nyumba salama zilizosababisha kuuwawa kwa wasio na hatia—ni jambo la kushangaza.

Sisi tunasisitiza haki ya kisheria na ya kikanuni ya kujilinda; haki ambayo Uislamu, sheria zote za mbinguni na sheria za kimataifa zimeithibitisha. Inawezekanaje yule anayetumia haki hii akalaumiwa, lakini mvamizi mkuu na kambi za kijeshi ambazo mashambulizi hutoka humo zikaachwa bila kulaaniwa?

Mambo ya msingi tunayotaka kuyaweka wazi:

Kwanza: Mashambulizi yaliyofanywa na vikosi vya Iran yalilenga tu maeneo ya kijeshi ambayo adui alikuwa akiyatumia kuishambulia ardhi ya Kiislamu, na kamwe hayakulenga miundombinu ya kiraia pekee.

Pili: Uwepo wa kambi za kijeshi za kigeni katika ardhi za nchi za Kiislamu, ambazo zinatumika kushambulia nchi nyingine ya Kiislamu, ni jambo la kuhuzunisha na unaweka nchi zinazozikaribisha katika hali ngumu mbele ya ndugu zao.

Tatu: Kuimarisha mshikamano wa ndani wa ulimwengu wa Kiislamu na kuzuia migogoro kati ya wana wa Umma ni dhamana ya kweli ya kukabiliana na vitisho vya nje. Migogoro ya ndani hunufaisha tu maadui wa Umma.

Wito kwa Rabitat al-‘Alam al-Islami:

Sisi tunaiomba Rabitat al-‘Alam al-Islami, kama taasisi ya Kiislamu ya kimataifa yenye hadhi, ikumbuke wajibu wake wa kisheria na kihistoria na isimame pamoja na wanyonge na waliodhulumiwa, si kuwa upanga dhidi yao. Wajibu wa kisheria unalazimisha kusimama upande wa haki na kusaidia waliodhulumiwa, na kabla ya kukosoa mwitikio wa aliyedhulumiwa, kumlaani mvamizi.

Tunauliza wazi: Ikiwa kambi za kijeshi katika ardhi za Kiislamu zitatumika kuishambulia nchi yenu, msimamo wa kisheria ambao Umma unapaswa kuchukua utakuwa upi?

Tunaiomba Rabitat al-‘Alam al-Islami:

1. Kurejea upya taarifa za hivi karibuni ambazo ndani yake msimamo wa Iran umeeleweka vibaya, na kujitahidi kutoa taarifa zinazounganisha badala ya kugawanya.

2. Kusisitiza katika taarifa zijazo juu ya haki ya kudumu ya nchi za Kiislamu kujilinda kisheria, usalama na mamlaka yao.

3. Kuhimiza mazungumzo ya moja kwa moja na yenye kujenga kati ya nchi za Kiislamu ili kutatua migogoro, na kushinikiza nchi zinazokaribisha kambi za kijeshi za kigeni kubeba wajibu wa kuzuia matumizi ya ardhi zao kwa ajili ya kushambulia nchi jirani za Kiislamu.

Umoja wa ulimwengu wa Kiislamu ni ngao imara mbele ya changamoto. Nasi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azikusanye safu za Waislamu, aondoe fitna miongoni mwao, na awaunganishe juu ya haki.

Na rehma na amani zimshukie Mtume wetu Muhammad na ahli zake na maswahaba wake wote.

Wanazuoni wa Ahl al-Sunnah wa Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha