Jumatatu 6 Aprili 2026 - 13:46
Kongamano la Kimataifa la Kupinga Ubeberu pamoja na maadhimisho ya Arubaini ya kiongozi shahidi lafanyika Qom Iran

Hawza: Kongamano la kimataifa la kupinga ubeberu katika fikra za kiongozi shahidi pamoja na maadhimisho ya Arubaini yake, litafanyika tarehe 17 Farvardin 1404 (6 April 2026) katika mji wa Qom Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Ofisi ya Mwakilishi wa Walii al-Faqih Azerbaijan ndani ys (Qom) itmeandaa kongamano la kimataifa lenye anuani ya “Kupinga ubeberu katika fikra za kiongozi shahidi” pamoja na hafla ya kuadhimisha Arubaini yake.

Katika kongamano hili, Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Sa‘iwar, mkuu wa Ofisi ya Mwakilishi wa Walii al-Faqih katika Azerbaijan, Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Husseini Kouhsari, Naibu wa Mawasiliano na Mambo ya Kimataifa wa Hawza, na Hujjat al-Islam wa al-Muslimin Qanbari, Naibu wa Mawasiliano na Mambo ya Kimataifa wa Jami‘at al-Mustafa, watatoa hotuba.

Tukio hili litafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 17 Farvardin 1404 (6 April 2026) saa 16:00 katika ukumbi wa mikutano wa Ahl al-Bayt World Assembly uliopo katika barabara ya Jamhuri ya Kiislamu, kati ya Jamhuri 4 na 6, mjini Qom Iran.

Kongamano la Kimataifa la Kupinga Ubeberu pamoja na maadhimisho ya Arubaini ya kiongozi shahidi lafanyika Qom Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha