Ijumaa 20 Machi 2026 - 23:10
Damu Safi ya Mashahidi Itaondosha Dhuluma na Ubeberu

Hawza/ Baraza la Juu la hawza limetoa salamu za rambirambi kufuatia shahada ya Dkt. Ali Larijani, Hujjat-ul-Islam wal-Muslimin Khatib, na Shahidi General Suleimani, huku likisema kuwa; damu safi ya mashahidi hawa na juhudi zao zisizo na kikomo zitazaa matunda na zitapindua mizinga ya dhuluma na ubeberu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Baraza la Juu la hawza ulisema hivi:

Bismillah al-Rahman al-Rahim

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.”

(Qur'ani, Surah al-Ahzab, 23)

Shahada ni zawadi kubwa ya kimungu kwa waja wema na wapiganaji wa kweli ambao wanajitolea maisha yao katika kuutetea Uislamu na heshima ya Waislamu.

Shahada ya mwanazuoni mchapakazi Dkt. Ali Larijani, Katibu Mkuu wa Baraza la Juu la Usalama wa Taifa, pamoja na mtoto wake mwaminifu na wenzake waadilifu, na vilevile shahada ya Hujjat-ul-Islam wal-Muslimin Hajji Sayyid Ismail Khatib, Waziri wa Habari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na Shahidi Generali Suleimani, Kamanda wa Jeshi la muqawama la Basij, katika vitendo vya kigaidi na uhalifu vya utawala wa Kizayuni na mtetezi wake Marekani, inapaswa kupokelewa rambirambi zetu na heshima kubwa.

Mwanazuoni mchapakazi Dkt. Ali Larijani anatoka katika familia ya kielimu na kidini, na aliyatumia maisha yake kwenye kutetea mfumo wa Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiutamaduni, vyombo vya habari na usalama wa taifa, alilinda ustawi wa Uislamu na Iran, na mwishowe alipata shahada akiwa katika mstari wa mbele wa muqawama dhidi ya maadui wa umma wa Kiislamu. Alijiunga na wenzake mashahidi, Imam Khomeini (rah) na kiongozi shahidi Ayatollah Khamenei (q.s).

Baraza la hawza, linatoa pole kwa Imam wa zama (as), Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, familia ya mashahidi, taifa kuu la Iran, vyuo vya kidini kote nchini, viongozi wa Serikali ya Kiislamu, na wapiganaji wote katika vita dhidi ya dhuluma na maadui wa Kiislamu.

Damu safi ya mashahidi hawa na juhudi zao zisizo na kikomo zitazaa matunda na kuangamiza mizinga ya dhuluma na ubeberu, na itasafisha njia ya ushindi wa upande wa haki, muqawama, na wenyekudhulumiwa duniani insha'Allah.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape daraja za juu mashahidi hawa na awaunganishie na waja wake wema, na kuliwezesha taifa la Iran na upande wa muqawama, kupata ushindi mkubwa dhidi ya maadui wa Uislamu na Waislamu.

Baraza la Juu la Hawza nchini Iran,
27 Esfand 1404/ 18 March 2026.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha