Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Siku ya Ijumaa, mamia ya waumini nchini Kenya walikusanyika katika Msikiti wa Kishia wa Parkroad mjini Nairobi, huku wakionesha mshikamano na upendo wao juu ya watu wa Palestina. Tukio hili la kihistoria limewashirikisha watu wa kila kizazi na hali hii ya mshikamano imekuwa ishara ya imani, haki, na ushujaa wa kuiunga mkono Palestina.
Siku ya Qudsi huadhimishwa duniani kote kila mwaka katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani, tukio lilianzishwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, Imam Ruhullah Khomeini (ra), kama wito wa mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya uhuru na haki za Wapalestina.
Waadhimishaji nchini Kenya walisema kuwa; kushiriki katika siku hii kunawakumbusha umuhimu wa mshikamano wa kidini na kimataifa, na kwamba kila mshikamano mdogo unaongeza sauti ya haki na kuendelea kudai amani kwa Wapalestina.
(Angalia picha za matukio ya siku hii hapa chini)










Maoni yako