Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatollah Javadi Amoli katika nasaha yake kwa walinganiaji amesema:
“Enyi waheshimiwa mnaokwenda kwa ajili ya tablighi, hakikisheni mnaendesha somo la tafsiri. Katika vikao vya jumla ambavyo mnatoa mihadhara, mnatumia aya za Qur’ani. Jitahidini pia kuwa na vikao vya faragha; kuweni sababu ya kuifanya Qur’ani iwe hai katika jamii. Tauhidi itakapokuwa hai katika jamii, mwanadamu aliye mwahhid kamwe hatabaki (bila msimamo). Haiwezekani kamwe kwa mgeni kudhani kwamba ataweza kuiangamiza nidhamu yetu na mapinduzi yetu…”
Darsa ya Tafsiri ya Suratu al-Qiyamah, kikao cha 5
02/11/1398 (Hijria Shamsia)
Maoni yako