Jumatatu 29 Desemba 2025 - 20:20
Iran ya ni mshika-bendera wa heshima na mpambanaji katika ulimwengu wa Kiislamu

Hawza/ Profesa Munawar Abbas, Rais wa Jumuiya ya Wahadhiri wa Vyuo vya Serikali vya Pakistan, katika warsha ya tano ya kimataifa isemayo: "Iran; Jukwaa la Heshima ya Kiislamu katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni," huku akisisitiza nafasi ya kimkakati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono Umma wa Kiislamu, alibainisha: Iran tangia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo, imekuwa na msimamo thabiti na wa kimsingi katika kuilinda Palestina na kukabiliana na uvamizi wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Profesa Munawar Abbas, Rais wa Jumuiya ya Wahadhiri wa Vyuo vya Serikali vya Pakistan, katika warsha-pepe ya tano ya kimataifa isemayo: "Iran; Jukwaa la Heshima ya Kiislamu katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni,"  iliyoandaliwa kwa juhudi za Majma‘u-l-‘Ālamī Qādimūn, aliitaja nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mizania ya kikanda na katika ulimwengu wa Kiislamu kuwa ya juu na yenye umuhimu mkubwa.

Profesa Munawar Abbas, akirejea nafasi ya Iran katika kuulinda Umma wa Kiislamu, alisema: Iran si tu katika eneo la Mashariki ya Kati, bali katika ulimwengu mzima wa Kiislamu inatambulika kama mshika-bendera wa heshima na mapambano, na imeendelea kuinga mkono Palestina tangu mwanzo wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo kwa namna endelevu.

Akigusia vitisho vya hivi karibuni vya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Iran, alisisitiza: Lengo kuu la vitisho hivi lilikuwa kubadilisha mfumo wa utawala na kuangamiza uwezo wa nyuklia na makombora ya Iran, lakini uzoefu wa vita vya siku 12 vya hivi karibuni umeonesha kuwa malengo haya hayakufikiwa.

Rais wa jumuiya ya Wahadhiri wa Vyuo vya Serikali vya Pakistan aliongeza: Licha ya mashinikizo makubwa ya kisiasa na vikwazo vya kiuchumi, Iran ina mshikamano wa ndani wa hali ya juu, na wananchi wake wamesimama kwa nguvu upande wa serikali yao.

Aidha, alibainisha kuwa: Hatua za kijeshi dhidi ya Iran hazikuishia tu kushindwa kuidhoofisha nchi hiyo, bali pia zilidhihirisha udhaifu na hali ya kuathirika ya utawala wa Kizayuni; utawala ambao ulikuwa ukijionesha kama alama ya hofu na uwezo wa kuzuia mashambulizi, lakini mbele ya Iran ulipatwa na mkanganyiko, hadi hata kuilazimisha Marekani kushinikiza kusitishwa kwa operesheni za kijeshi.

Profesa Munawar Abbas, akisisitiza mtazamo wa kimsingi wa Iran katika kuunga mkono mapambano ya Palestina na harakati za muqawam katika eneo, alisema: Misaada hii inapaswa kuwa chachu ya umoja wa Umma wa Kiislamu na kuzuia kugeuka kuwa sababu ya migogoro ya kidini na kisiasa.

Katika kuendelea, akirejelea mabadiliko mapya ya kikanda, alisema: Iran leo haiko peke yake, Umma wa Kiislamu, ikiwemo Pakistan, umesimama pamoja na nchi hii. Nchi za Kiislamu zinapaswa badala ya kushindana na kukabiliana, kuchagua njia ya ushirikiano, uwiano na mshikamano kwa ajili ya kulinda uthabiti wa eneo.

Rais wa jumuiya ya Wahadhiri wa Vyuo vya Serikali vya Pakistan alihitimisha kwa kusisitiza: Iran kwa kushikamana na misingi ya Kiislamu na kuunga mkono muqawama, imetoa mfano wa kivitendo kwa ulimwengu wa Kiislamu, na hatua yoyote ya kijeshi au ya vikwazo dhidi yake haitazaa matokeo mengine isipokuwa kuongeza hali ya kutokuwa na utulivu na migogoro katika eneo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha