Jumatatu 29 Desemba 2025 - 22:31
Maktaba ya Shahidi Sulaimani ni ramani ya njia ya Qur’ani katika ushindi wa Muqawama

Hawza/ Sheikh al-Daqqaq, akisisitiza misingi ya Qur’ani ya maktaba ya Muqawama, alisema: Maktaba ya Shahidi Haj Qasim Sulaimani, kwa kutegemea uchambuzi wa kimkakati, malezi ya rasilimali watu na utii kwa uongozi (wilayah), imechora ramani iliyo wazi ya kutekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya uokovu na ushindi wa Jabhah ya Muqawama dhidi ya Jabhah ya Uistikbari.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Mashhad, Sheikh Abdullah al-Daqqaq, mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya ya kukurubisha madhehebu ya kiislamu, jioni ya Jumamosi tarehe 27 December, katika kongamano la pili la kimataifa la Al-Ghalibūn lililokuwa na anuani isemayo "Maktaba ya Shahidi Sulaimani; Njia Iliyowazi ya Muqawama," lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli Aftab-e-Wilayat, kwa kubainisha vipengele vya Qur’ani, kimkakati na kistaarabu vya Muqawama, alisisitiza umuhimu wa Jabhah ya Muqawama kuvuka hatua ya kauli mbiu na kuingia katika uwanja wa vitendo.

Taswira ya Qur’ani ya Hizbullah na ahadi ya hakika ya uokovu

Akirejelea aya za Qur’ani Tukufu kuhusiana na Hizbullah, alisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur’ani, anapofafanua na kuielezea Hizbullah, anawatambulisha kama waokokaji wa kweli. Uokovu huu si dhana ya kinadharia au ya Akhera pekee, bali una njia, viashiria na vielelezo vya wazi katika uwanja wa kijamii na kisiasa wa Umma wa Kiislamu; na ni lazima kujiuliza: uokovu huu unapatikana vipi na kupitia njia ipi?

Mwakilishi wa Kiongozi wa Waislamu wa Kishia wa Bahrain, akitaja vielelezo halisi vya kutimia kwa Hizbullah katika zama za sasa, alisisitiza: Tunachokiona leo katika shakhsia na mchango wa Shahidi mkubwa Haj Qasim Sulaimani nchini Iran, Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis nchini Iraq, Sayyid Hassan Nasrallah nchini Lebanon, wanajihadi na viongozi wa Muqawama nchini Yemen, pamoja na msimamo wa wananchi na mashahidi wa Palestina—haya yote ni vielelezo dhahiri na halisi vya Hizbullah kwenye Qur’ani ambayo Mwenyezi Mungu ameahidi ushindi na uokovu kwao.

Sheikh al-Daqqaq, akisisitiza kwamba ushindi katika mantiki ya Muqawama ni zao la harakati iliyoratibiwa na yenye malengo, alisema: Uzoefu wa Muqawama umeonesha kuwa, bila ramani ya njia, uchambuzi sahihi wa hali na utambuzi wa uwezo uliopo, haiwezekani kufikia ushindi wa kudumu. Kwa hiyo, Muqawama unahitaji misingi na nguzo zilizo wazi zitakazoufikisha kwenye kituo cha uokovu.

Nguzo tatu kuu za maktaba ya Muqawama

Akifafanua kanuni tatu za msingi katika maktaba ya Muqawama, aliongeza: Kanuni ya kwanza ni uchambuzi wa kimkakati na upangaji wa kimkakati. Harakati ya Muqawama inayoweza kuchambua kwa usahihi mazingira, adui, fursa na vitisho, na ikaweka mipango juu ya msingi huo, tayari imepiga hatua katika njia ya mafanikio.

Daqqaq aliitaja kanuni ya pili kuwa ni mshikamano wa nguvu na malezi ya rasilimali watu, na akaendelea: Kulea nguvu kazi waumini, wenye ufanisi na ufahamu—hasa kutoka miongoni mwa kizazi cha vijana—na kuwaandaa kwa majukumu ya baadaye, ni nguzo ya msingi ya kila harakati yenye ushindi. Muqawama bila rasilimali watu iliyoratibiwa na kufunzwa, hautafikia matokeo yanayotarajiwa.

Alisema utii kwa uongozi na kunyenyekea kwa uongozi wa Mwenyezi Mungu kuwa nguzo ya tatu, na akasema: Umoja wa Jabhah ya Muqawama unatokana na ufuasi wa uongozi wenye ufahamu. Popote kanuni hii ilipohifadhiwa, Muqawama ulipata ushindi; na popote ilipodhoofishwa, majeraha na matatizo yalianza.

Mahitaji ya kimuundo ya sasa ya Muqawama

Sheikh al-Daqqaq, akirejea hali ya sasa ya eneo na mashinikizo ya pande zote za adui, alibainisha kuwa: Leo Jabhah ya Muqawama ina haja ya kina na ya dharura ya kuunda miundo iliyoratibiwa na ya kimkakati. Muundo wa kwanza ni kituo cha upangaji wa kimkakati, ambacho jukumu lake ni kubuni njia ya harakati na kutekeleza malengo makuu ya Muqawama.

Aliongeza: Muundo wa pili ni kituo cha mafunzo na malezi ya rasilimali watu—hasa vijana—kwa mtazamo wa utafiti wa baadaye, ili Muqawama uweze kulea nguvu kazi yenye uwezo na basira kwa ajili ya kesho yake. Muundo wa tatu ni kituo cha uchakataji wa taarifa na uunganishaji wa rasilimali, ambacho kama mkono wa utekelezaji, kitaelekeza uwezo na mali za Muqawama kuelekea malengo ya juu.

Mwakilishi wa Kiongozi wa Waislamu wa Kishia wa Bahrain, akigusia nafasi ya kipekee ya Shahidi Haj Qasim Sulaimani, alisisitiza: Haj Qasim Sulaimani alikuwa kiungo cha kuunganisha vituo hivi vitatu na kazi hizi tatu za msingi. Kwa upande mmoja, kwa mtazamo wake wa kimkakati aliweza kuona upeo kwa usahihi; kwa upande mwingine, kwa kulea na kuratibu rasilimali watu waumini na mashujaa, aliimarisha uti wa mgongo wa Muqawama; na hatimaye aliweza kuweka pamoja rasilimali na uwezo wote wa nchi za mhimili wa Muqawama katika njia ya kuzikomboa ardhi na kufufua heshima ya mataifa.

Sheikh al-Daqqaq, akichambua sababu ya uadui mkali wa Ubeberu dhidi ya makamanda wa Muqawama, alisema: Ikiwa makamanda kama Haj Qasim Sulaimani, Abu Mahdi al-Muhandis na viongozi wengine wa Muqawama walilengwa kwa mauaji na kufikia shahada, ilikuwa ni kwa sababu walibeba mtazamo huu wa kina wa kimkakati na kistaarabu—mtazamo uliovuruga hesabu za adui na kuutikisa msingi wa utawala wa kibeberu.

Dhamira ya kihistoria ya leo ya Umma wa Kiislamu

Akisisitiza juu ya wajibu wa kihistoria wa waliokuwepo na wanaharakati wote wa Jabhah ya Muqawama, alisema: Leo ni wakati wa kuvuka maneno na kuingia katika uwanja wa vitendo. Kila mmoja wetu ana jukumu la kihistoria, na ikiwa tunataka kupiga hatua katika njia hii, ni lazima tuinue akili yetu ya kimkakati, tujitahidi katika malezi ya rasilimali watu na kutoa kipaumbele maalumu kwa vijana, na tuunganishe uwezo wote katika mfumo wa harakati ya jihadi iliyoratibiwa.

Mjumbe wa Majma‘u-l-‘Ālamī li-Taqrīb Bayna-l-Madhāhib al-Islāmiyya alihitimisha kwa kusema: Kila atakayejitahidi katika kutekeleza kanuni hizi na kuunda miundo hii ya kimkakati, bila shaka atakuwa askari wa jeshi la waandaaji wa mazingira ya kudhihiri kwa Imam wa Zama (a.j.), na ahadi ya Mwenyezi Mungu ya nusra, heshima na uokovu itamfikia.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha