Jumatatu 29 Desemba 2025 - 19:09
Hatua ya awali ya mashindano ya Qur’ani Tukufu nchini Oman yakamilika

Hawza/ mashindano ya awali ya Qur’ani Tukufu yaliyoandaliwa kwa ufadhili wa Wizara ya Wakfu ya Oman na kwa ushiriki wa zaidi ya wahifadhi na wasomaji wa Qur’ani 170 yamekamilika.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, shindano hili limefanyika kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha nafasi ya Qur’ani Tukufu, kuunga mkono madrasa za Qur’ani kama waongoza jamii ya leo, na kama msingi wa elimu na imani katika jamii.

Shindano hili pia liliandaliwa na Wizara ya Wakfu ya Oman kwa lengo la kuwaandaa zaidi washiriki kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Qur’ani ya ndani ya nchi na ya kimataifa, pamoja na kukuza maadili kama vile ikhlasi.

Taasisi hii inalenga kuwahamasisha vijana wa Kioman kushikamana zaidi na Qur’ani Tukufu kupitia kuhifadhi, kuelewa na kutafakari aya zake, na inajitahidi kuhakikisha kuwa, vijana wanazifanya aya za Qur’ani kuwa kama ubao ulio mbele yao katika maadili na vitendo vyao.

Chanzo: Observer

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha