Jumapili 28 Desemba 2025 - 17:10
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf atahadharisha dhidi ya minong’ono ya kuhalalisha uhusiano na Israel

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji amesema kuwa: yaliyotajwa katika hotuba ya Sako (Askofu wa Wakristo wa Kaldani wa Iraq) kuhusiana na kuhalalisha uhusiano na Israel, hayakubaliki kabisa na ni yenye kupingwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Swala ya Ijumaa alizozitoa kwenye Husseinia Kubwa ya Fatimiyya mjini Najaf Ashraf, alisema kuwa: yaliyosemwa katika hotuba ya Sako (Askofu wa Wakristo wa Kaldani wa Iraq) kuhusu kuhalalisha uhusiano na Israel ni kwamba; mazungumzo yoyote yenye asili ya kisiasa kwenye mwelekeo huu hayakubaliki kabisa na yanakataliwa, yanapingana na sheria za Iraq, na yanastahiki kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aliongeza kusema: hata kama mazungumzo kama hayo yataelezewa kwa sura ya kibinadamu, basi yule anayezungumza juu ya ubinadamu anapaswa kusimama na kufikiri kwa kina mbele ya zaidi ya mashahidi sitini elfu wa Palestina, pamoja na makumi ya maelfu ya wanawake na watoto waliopotea ambao bado wako chini ya vifusi; sambamba na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Syria na Lebanon.

Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf aliuliza kwa kusema: inawezekanaje kupuuzwa ukweli wa kwamba; Israel kwa ushahidi wa kimataifa, imegeuka kuwa utawala wa kigaidi?

Ziara ya Rais wa Pakistan katika Ataba Tukufu

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji alielezea ziara ya Rais wa Pakistan katika Ataba Tukufu za Iraq na kusema: Ziara hii inaakisi dalili za kuenea kwa Ushia duniani, kurejea kwa ulimwengu wa Kiislamu katika kifua cha Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao), kushindwa kwa fikra zinazowapinga, na kufikia mwisho kwa zama za kusambaza ujinga, kupotosha na kukufurisha.

Kuondolewa Golan katika ramani ya Syria

Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf pia aligusia kile kilichotangazwa rasmi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria kuhusu kuondolewa Golan katika ramani ya Syria, na kusema: kwa upande mwingine, Waziri wa Ulinzi wa utawala wa Israel ametangaza kwamba hatarudi nyuma wala kutoka Syria wala kutoka Ghaza, na hutaiacha ardhi ya Golani hata milimita moja.

Kwa kuuliza, ni kwa nini hakuna msimamo unaochukuliwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu au wale wanaounga mkono kuhalalisha uhusiano na utawala wa Israe?l, alielezea tukio hili kuwa ni ishara ya njama za wazi kati ya serikali ya sasa ya Syria na mkoloni Muisraeli, na akakumbusha ukweli wa kile kinachoitwa “serikali mpya ya Julani”.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha