Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali al-Khatib, Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon, katika taarifa yake amelaani vikali uvamizi wa mara kwa mara unaofanywa na Israel dhidi ya Lebanon.
Amebainisha kuwa vitendo hivi ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya Lebanon na kuheshimu raia, na kwamba vinaunda mlolongo wa kihalifu. Mifano ya hivi karibuni ya uhalifu huu ni mauaji ya Ain al-Hilweh na uvamizi wa al-Tayri, ambako jinai za Kizayuni zimewalenga raia wasio na hatia, vijana, watoto na wanafunzi wa vyuo na shule.
Sheikh al-Khatib amesema kuwa operesheni hii ya kigaidi iliyoratibiwa ni uvamizi wa Lebanon na wa Walebanoni wote wanaowajibika kuonesha mshikamano na watu na ndugu zao katika taifa.
Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia ameongeza: “Tunaziwasilisha jinai hizi zinazoendelea mbele ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa, nchi rafiki na ndugu, na Kamati ya Kifundi, na tunaziomba zichukue misimamo madhubuti ya kulaani vitendo hivi vya kinyama na kusimamisha uvamizi huu unaoendelea dhidi ya watu wetu; kwani hairuhusiwi watoto na raia kuwa mawindo ya unyama wa Israel unaolingana na mauaji yanayoendelea Ghaza.”
Ameitaka pia Serikali ya Lebanon kutekeleza majukumu yake na kubeba dhima katika kusimamisha mauaji ya watoto wa taifa lake. Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka katika majukwaa ya kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na kupitia balozi zake nje ya nchi ili kufichua uhalifu wa Kizayuni, kuonesha mshikamano na wahanga na majeruhi, na kutumia kila njia kuzuia uvamizi unaoendelea dhidi ya Lebanon.
Mwisho wa kauli yake, Sheikh al-Khatib ametoa mkono wa pole wa dhati kuzielekea familia za mashahidi ambao “tunawaamini kuwa wako hai na wanaruzukiwa kwa Mola wao.” Amewaombea rehema kwa Mwenyezi Mungu, na kwa familia zao amewaombea subira na utulivu, na amewaombea majeruhi wapate kupona haraka.
Maoni yako