Jumapili 16 Novemba 2025 - 23:02
Sheikh Ibrahim Zakzaky Akutana na Kiongozi wa Tariqa ya Qadiriyya Nigeria, Sheikh Ibrahim Isa Makwarari

Hawza/ Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ibrahim Zakzaky, amempokea Sheikh Ibrahim Isa Makwarari, kiongozi wa Tariqa ya Qadiriyya Nigeria, pamoja na ujumbe wake, katika makazi yake mjini Abuja.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, katika muendelezo wa jitihada za kuimarisha umoja miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu nchini Nigeria, Sheikh Ibrahim Isa Makwarari, kiongozi wa Tariqa ya Qadiriyya Nigeria, akiwa na msafara wa wafuasi wake, alikutana na kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ibrahim Zakzaky, katika nyumba yake mjini Abuja.

Katika mkutano huo, Sheikh Ibrahim Isa alieleza hisia zake za kuungana na Sheikh Zakzaky na akakumbusha tukio la kuuawa kishahidi zaidi ya wanafunzi na wafuasi wake 1,000 katika mauaji ya umwagaji damu ya mwaka 2015 huko Zaria, yanayojulikana kama “Tukio la Buhari”, wakiwemo watoto wake watatu. Pia alikumbushia kuhusu kuuawa kishahidi kwa watoto wengine watatu wa Sheikh Zakzaky na kundi la wafuasi wake mwaka 2014, wakati wa utawala wa Goodluck Jonathan.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, naye, huku akiwakaribisha wageni kwa heshima na kuonesha furaha yake kwa ziara ya kiongozi wa Tariqa ya Qadiriyya, alisisitiza umuhimu wa mshikamano kati ya madhehebu na harikati za Kiislamu nchini Nigeria.

Mwishoni mwa mkutano huu, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria aliwapa wajumbe wa Qadiriyya zawadi zenye baraka zinazohusiana na Ahlul-Bayt (as). Wageni, kwa upande wao, walishukuru kwa mapokezi ya dhati na ya joto kutoka kwa Sheikh Ibrahim Zakzaky na wakautaja mkutano huo kuwa wenye mafanikio.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha