Jumamosi 15 Novemba 2025 - 22:38
Kujisalimisha hakupo katika kamusi yetu/ Utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano ni hatua ya kuanzia katika mjadala unaohusu mkakati wa usalama wa taifa

Hawza/ Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni unaendelea, kwa msaada na ushiriki wa Marekani, kufanya mashambulizi yake ya kila siku dhidi ya Lebanon.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ali Damuush, Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon, katika mkutano wake na kundi la mabaraza ya mitaa katika Kituo cha Imam Mujtaba (as) huko Dhahiyya  Beirut Kusini, alisisitiza kuwa; utawala wa Kizayuni unaendelea kwa msaada na ushiriki wa Marekani kufanya mashambulizi yake ya kila siku dhidi ya Lebanon, na wakati huohuo kuna juhudi za kuwazingira na kuwatenga ya watu wa muqawama ili kudhoofisha ari ya uvumilivu na kusimama imara miongoni mwa wananchi.

Akasema: Leo Lebanon iko mbele ya machaguo mawili; kuendelea na mauaji na kuzingirwa kila siku au kujisalimisha mbele ya masharti ya adui. Ingawa sisi hatutafuti vita, lakini kujisalimisha hakupo katika kamusi yetu.

Sheikh Damuush alikumbushia kuwa vita vilisitishwa tarehe 27 Novemba 2024 kulingana na makubaliano ambayo serikali ya Lebanon ilifikia. Makubaliano hayo yalisisitiza kusitisha vitendo vya uhasama na kurudi nyuma kwa adui kutoka maeneo aliyo yavamia, na Hizbullah pia iliyakubali na kuyatekeleza. Lakini utawala wa Kizayuni tokea siku ya kwanza haujayatekeleza, na umefikisha idadi ya uvamizi wake zaidi ya kesi elfu tano, mbele ya macho ya walimwengu na kwa uungeaji mkono dhahiri wa Marekani.

Akaongeza kuws: Pamoja na uvamizi huu wote, adui hajawahi kufanikiwa kuidhoofisha ari ya kusimama imara ya wetu ambao wameshikamana na ardhi yao, usalama wao, utulivu wao na heshima yao.

Mjumbe huyu mwandamizi wa Hizbullah, huku akibainisha kuwa bila kujali utendaji wa sasa wa serikali na baadhi ya viongozi, hatua ya sasa inahitaji serikali kubeba wajibu wake kikamilifu, alisema: Daima tumekuwa tukitaka kuwepo serikali imara na ya haki; serikali ambayo watu wake wana imani nayo, inayotetea masuala yao na kulinda mamlaka ya nchi.

Akaendelea: Leo serikali inasema kuwa inataka kubeba wajibu na kuna makubaliano yaliyopo ambayo utekelezaji wake uko mikononi mwa serikali. Serikali hii ina njia rasmi ya mawasiliano kupitia Kamati ya Uangalizi wa Kusitishwa Mapigano, na ni lazima kutumia njia hiyo kumlazimisha adui kutekeleza makubaliano.

Sheikh Damuush alisisitiza kwamba: Mradi tu adui hajachukua hatua zinazotakiwa kutekeleza ahadi zake, Lebanon hailazimiki kutafuta hatua mpya wala makubaliano mbadala. Pia, sehemu ya kuingilia kwa njia ya asili kwa ajili ya mazungumzo ya kitaifa kuhusu mkakati wa usalama wa taifa wa Lebanon ni utekelezaji kamili wa makubaliano ya 27 Novemba na kusimamisha uvamizi.

Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, akirejea maumivu na mateso yanayoendelea kwa watu wa Lebanon, alisema: Pamoja na majeraha, mateso na damu iliyomwagika, hatua hii inahitaji ushirikiano, subira na busara. Muqawama wetu una hekima ya kutosha, ujasiri na basira ya kufanya maamuzi yanayolingana na mazingira ya sasa.

Kuhusu suala la ujenzi upya wa maeneo yaliyoharibiwa na uvamizi wa hivi karibuni, alisema kuwa; Hizbullah inafanya kazi katika njia mbili. Akaeleza: Katika njia ya kwanza, Hizbullah kwa kulipa fidia kwa walioathirika, inatimiza jukumu lake la kisharia na kimaadili kwa wananchi wake; tumekamilisha jalada kubwa ambalo serikali haina uwezo wa kulifanya; tumefanikiwa kukarabati takribani vitengo 370,000 vya makazi na wamiliki wao wamerejea katika nyumba zao, na maelfu ya familia ambazo nyumba zao zilibomolewa. Hii ni hatua ya kwanza ya ujenzi upya inayohitaji kuendelea katika upande wa ukarabati na makazi, hasa katika vijiji vya kusini na vya mipakani.

Sheikh Damuush akaongeza: Pamoja na juhudi za kuzingirwa, ya mwisho ikiwa ni masharti na taratibu zilizowekwa na ujumbe wa Wizara ya Hazina ya Marekani. Kile Marekani inachokifuatilia hakika ni udhibiti wa wazi juu ya Lebanon na ukiukaji mkubwa wa mamlaka ya taifa. Lengo la moja kwa moja la shinikizo hili ni kuzuia ujenzi mpya. Lakini pamoja na changamoto hizi zote, tutaendelea na ujenzi na tutajulisha undani wa hatua zinazofuata kwa wakati muafaka.

Kuhusu njia ya pili, alisema: Njia hii inafuatwa kupitia serikali. Tumejitahidi sana katika msingi huu kwa ufahamu kuwa kuna uamuzi wa kisiasa wa wazi wa kuweka vikwazo mbele ya ujenzi mpya, kwa kuwa Washington inaweka shinikizo moja kwa moja kwa nchi zinazotaka kutoa misaada. Pamoja na haya, wajibu wa serikali ni kubeba jukumu la jalada la ujenzi mpya. Kile kilichofanyika hadi sasa ni hatua za awali tu; kuanzia kupitishwa kwa sheria za misamaha na ujenzi, hadi kuweka utaratibu wa ulipaji fidia na jinsi ya kutumia fedha hizo—ambazo ndizo zinazounda mfumo wa kisheria. Kwa upande wa miundombinu pia baadhi ya miradi imetekelezwa kupitia Baraza la Kusini na taasisi rasmi kama vile umeme na maji.

Mjumbe wa Hizbullah Lebanon alibainisha kuwa mkopo wa thamani ya dola milioni 250 kutoka Benki ya Dunia unasubiri kupitishwa na bunge, lakini hatua hizi zote bado hazijafikia hatua ya kufadhili nyumba zilizoharibiwa na kuandaa mpango wa kina wa ujenzi wa vijiji vya mipakani ambavyo adui anajaribu kuviacha bila wakazi. Huu ni mtihani mkubwa tunaokabiliana nao kwa lengo la kuwaweka watu wao katika ardhi na nyumba zao.

Sheikh Damuush, akimaliza hotuba yake huku akishukuru juhudi za mabaraza na manispaa, alisema: Hakuna shaka kwamba manispaa zimefanya juhudi kubwa, pamoja na upungufu wa vifaa, zimejitolea nafsi na nguvu kurejesha maisha ya kawaida kwenye vijiji vilivyoathirika. Sisi pia tutakuwa pembeni mwenu ili kwa ushirikiano na mshikamano, tuijenge tena nchi yetu na vijiji vyetu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha