Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, inatarajiwa kuwa kipindi hiki kitarushwa hewani kila wiki siku za Ijumaa na Jumamosi kupitia vituo vya televisheni vya Al-Hayat, CBC, Al-Nas, pamoja na mtandao wa Watch IT.
Zaidi ya washiriki na wasomi wa Qur’ani 14,000 kutoka maeneo mbalimbali ya Misri wameshiriki katika mahojiano ya awali ya kipindi hiki kwa ajili ya usajili. Mfululizo huu wa vipindi vya Qur’ani unatayarishwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Awqaf ya Misri na Taasisi ya Umoja wa Huduma za Habari.
Jopo la majaji wa kipindi hiki limechaguliwa kutoka miongoni mwa watu mashuhuri wa kidini na wa kitaaluma wa Misri na pia kutoka ulimwengu wa Kiislamu, akiwemo Sheikh Hassan Abd al-Nabi, naibu wa Kamati ya Ukaguzi wa Qur’ani ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar; mtaalamu wa sauti na makamat, Dkt. Taha Abd al-Wahhab; Mustafa Hosni, mtaalamu wa masuala ya Kiislamu; na qari mashuhuri Sheikh Taha al-Numani.
Chanzo: Shirika la Habari Misr al-Youm
Maoni yako