Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya SShirika la Habari la Hawza, Guardiola katika ujumbe wa video ambao tayari umesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kutazamwa na watu wengi, alisema: “Mchezo huu ni kutoa heshima kwa roho za zaidi ya wanamichezo 400 wa Kipalestina waliouawa kishahidi huko Ghaza.” Alisisitiza kuwa tukio hili ni zaidi ya mpira wa miguu, na kimsingi ni alama ya sauti ya watu hawa na mshikamano pamoja nao.
Mchuano huu ni mchezo wa hisani ambao timu ya Catalonia itachuana na timu ya taifa ya Palestina. Lengo lake ni kuunganisha michezo yenye afya na roho ya kibinadamu na kuunga mkono waliodhulumiwa. Mapato yote yatokanayo na uuzaji wa tiketi yataelekezwa moja kwa moja kusaidia misaada ya kibinadamu na miradi muhimu ya kijamii nchini Palestina, na yanatarajiwa kuwasaidia wale walioathirika na vita vinavyoendelea Ghaza.
Bila shaka, mchezo huu pia una thamani kubwa ya kiufundi kwa timu ya Palestina, kwani kukutana kwa timu hiyo na timu ya Catalonia itakuwa fursa muhimu kwa Palestina kujiandaa kwa mchezo wa mchujo wa Kombe la Kiarabu dhidi ya Libya, utakaofanyika tarehe 25 Novemba huko Doha, Qatar. Guardiola alisisitiza kuwa mchezo huu ni mazoezi ya kimfano na kiufundi, unaowapa wachezaji nafasi ya kupata uzoefu chini ya presha huku ukikuza pia ujumbe wa amani.
Chanzo: Roya News
Maoni yako