Jumapili 16 Novemba 2025 - 22:55
Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan: Ghaza bado iko katika giza la dhulma

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika ujumbe wake, amesisitiza kuwa licha ya kuwa subira ni haja ya kimaumbile ya binadamu, dunia bado iko mbali na kuitimiza, na Ghaza ndiyo mfano ulio wazi wa ukosefu huu wa haki.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika ujumbe alioutoa kutokana na mnasaba wa tarehe 16 Novemba, Siku ya Kimataifa ya Uvumilivu na Subira, alisisitiza ulazima wa ustahamilivu kama hitaji la msingi la kibinadamu na wito wa fitra. Akiashiria kuwa zaidi ya miaka nane ya muongo imepita tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, alisema kuwa dunia bado iko mbali na kutekeleza kwa hakika thamani hii ya kuvumiliana na kustahimili, jambo linaloonesha kushindwa kwa lengo hili la msingi.

Akinukuu mateso ya watu wa Palestina, alibainisha kiwa: Katika siku ambayo imesajiliwa kama Siku ya Kimataifa ya Uvumilivu, Wapalestina wa Ghaza bado wako chini ya dhulma na mzingiro, na usiku mchungu wa uonevu unaendelea kulazimishwa juu yao. Lau roho ya uvumilivu ingekuwa imetawala katika jamii za kibinadamu na lau kukingekuwa na kusimama imara dhidi ya dhulma ya Wazayuni, dunia leo angalau ingekuwa na kiasi fulani cha utulivu na uthabiti.

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistan, akiukosoa Umoja wa Mataifa, alisema: Umoja wa Mataifa hadi sasa umeshindwa kufanya mageuzi ya ndani ya taasisi yake na kuhifadhi nafasi yake ya kweli kama chombo kikuu cha kimataifa. Uingiliaji na ubabe wa mataifa makubwa umeharibu hadhi ya taasisi hii, na kusababisha maeneo mengi duniani, ikiwemo Palestina, kuendelea kuwa uwanja wa dhulma, ghasia na ukosefu wa uvumilivu.

Akiendeleza hoja yake, alisema: Uvumilivu ni mhimili wa wastani wa kijamii na ufunguo wa utulivu katika maisha ya pamoja. Dini zote za mbinguni zimesisitiza juu yake, na kwenye Uislamu, kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna, nafasi yake ni ya juu na ya msingi. Jamii inaweza tu kufikia mizani pale heshima ya pande zote, kuvumilia maoni tofauti na kustawisha roho ya kijamii ya kustahamiliana kunapowekwa ndani ya mifumo yake.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, akigusia falsafa ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, alibainisha: Miaka nane ya muongo iliyopita, lengo la kuanzishwa kwa taasisi hii lilikuwa kulinda haki za binadamu, kukabiliana na uvamizi na ubabe, na kupunguza mivutano baina ya mataifa; lakini kwa masikitiko, utendaji wake haujaenda sambamba na malengo yake ya awali. Umoja wa Mataifa unapaswa kuwa alama ya haki na usawa, si chombo cha nguvu za mataifa maalumu.

Akaongeza pia: Katika utekelezaji wa Kuamrisha mema na kukatana maovu, kanuni ya kwanza ni kuzingatia uvumilivu na subira; viongozi na watawala wanaopewa mamlaka wana wajibu wa kuunda mazingira yenye afya na ya kujenga katika jamii. Bila kuimarisha roho ya ustahamilivu na heshima ya pande zote, haiwezekani kupunguza misuguano ya kijamii na kuzuia kuibuka kwa mazingira ya ukandamizaji. Ni kwa kushikamana na kanuni hizi tu ndipo jamii inaweza kupiga hatua katika njia ya wastani, maendeleo na uimara.

Inafaa kutajwa kuwa Umoja wa Mataifa, kutokana na umuhimu wa thamani za kibinadamu na ulazima wa kueneza utamaduni wa amani na kuishi kwa maelewano, uliitangaza tarehe 16 Novemba kama Siku ya Kimataifa ya Uvumilivu na Subira ili ujumbe wa ustahamilivu, heshima na udugu usambae duniani kote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha