Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad al-Qattan, mwenyekiti wa Jumuiya ya Qawluna wal-Amal na mwanazuoni wa Kisunni nchini Lebanon, katika msimamo wake wa kisiasa kutoka mji wa Bar Elias katika eneo la Bekaa, alisisitiza kuwa: “Imani yetu ni mojatu nayo ni kwa taifa letu; na adui wetu ni mmoja — adui wa Kizayuni ambaye hana chembe ya utu.”
Alionesha masikitiko yake juu ya uwepo wa baadhi ya watu miongoni mwa “wenzeke katika taifa” ambao wanaposoma, wanasoma tu kitabu cha adui; na wanapoona, wanaona tu kwa macho ya adui. Akasema kuwa watu hawa hawatambui ulazima wa kuwa imara na kubakia Lebanon — jambo ambalo ni lazima ili kuilinda nchi yetu mbele ya changamoto zote.
Sheikh al-Qattan alisema kwamba tajriba zetu na adui huyu zinaonesha wazi kwamba yeye ni adui wa ubinadamu; kile alichokifanya Palestina kinaonesha kwa uthabiti ukatili wake, na kwamba hana utu wala huruma.
Mwanazuoni huyo wa Kisunni wa Lebanon aliongeza kwa kusema: “Tunawaambia watu hawa kuwa sharti mrudi mkahakiki upya misimamo yenu; na msome ‘kitabu cha utukufu na heshima’ — kitabu kinachotufundisha kuwa katika kukabiliana na adui huyu lazima tuwe imara, tuwe na umoja wa kitaifa na Kiislamu, na tuilinde nguvu yetu na kuilinda jamii yetu iliyo moja.”
Maoni yako