Jumatatu 27 Oktoba 2025 - 22:45
Uchaguzi wa Iraq: “Mapigano Meupe” ya Taifa katika Kuilinda Dhamira ya Muqawama

Hawza/ Katika mwelekeo wa uchaguzi wa Iraq, Abu Alaa al-Wala’i alisema kuwa uchaguzi wa Iraq ni “mapigano meupe” ya kiwango kamili; silaha yake ni kura safi za taifa na uwanjani ni sanduku la kura, ambapo taifa letu la muqawama litashinda.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid ash-Shuhada na Muqawama wa Kiislamu ya Iraq, katika sherehe ya kuadhimisha kumbukumbu ya shahada ya kiongozi wa muqawama, Sayyid Hassan Nasrallah, akitoa maelezo kuhusu hadhi na nafasi ya kiongozi huyo alisema kuwa; siku ya shahada ya Sayyid Nasrallah (ra) imegeuka kuwa tukio la kuhuisha sifa zote, kukumbusha thamani zote na kuakisi utu wote.

Aliongeza kuwa: shahidi wa umma, shahidi Nasrallah, ni mkombozi wa kambi ya Huseinn (a.s), mwanafunzi mwaminifu wa mtaala wa Ali (a.s) na mfano hai miongoni mwa wafuasi wa Imam Mahdi (aj).

Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid ash-Shuhada alisema kuwa katika imani yake alikuwa kama Abu Dharr, katika uaminifu wake alikuwa kama Salman Muhammadi, na katika ujasiri wake alikuwa kama Malik al-Ashtar. Akabainisha kuwa iwapo mashahidi wa zama hizi kama Suleimani, al-Muhandis na Sayyid Haider al-Mousawi wangeishi enzi za Mtume na Ahlul-Bayt (as), basi hadithi na miujiza ingezungumziwa kuwahusu wao.

Akitaja kuwa adui anapolichagua taifa lako kama lengo, hiyo inaonesha kuwa wewe ni kikwazo mbele ya miradi yake ya ukoloni, hasa katika eneo na Iraq. Aliongeza: ninaamini damu ya Sayyid Hassan itafutilia chini viti vya watawala wa dhulma na serikali za waasi; tangis kuibuka kwa tufani ya al-Aqsa, imani yetu ya juu ya kutoepukika kwa ushindi dhidi ya wakoloni haijawahi kupungua hata kidogo.

Abu Alaa al-Wala’i alisema: iwapo Wamarekani na Waarabu wa Kizayuni wangeweza kukumbana na upinzani wa watu wa Palestina ikiwa imara, basi wangechagua mazungumzo ya moja kwa moja; adui hajafanikiwa kwenye vita, mashambulio ya anga au njaa ili kufikia malengo yake. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa wateule wake waaminifu, katika kusonga kwenye ushindi.

Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid ash-Shuhada asema: ushindi uliotajwa na Mwenyezi Mungu kwa waumini ni wa hakika, ili mradi tu uwe pamoja na subira, tawakkul (kumtegemea Allah), imani kwa Mwenyezi Mungu, pamoja na nia thabiti, ujasiri na uvumilivu.

Akibainisha kuwa ;uchaguzi huu ni tofauti kabisa na chaguzi zote ziliyopita kutokana na matumizi ya zaidi ya fedha za kisiasa, alisema: natumai katika vikao vijavyo bunge litapitisha sheria ya kikatiba itakayozuia utambulisho wa idadi ya wagombea kuongezeka mara mbili kutokana na mabadiliko yeyote ya vyama — kwa mfano, katika Basra kuna viti ishirini na tano (25), hivyo kila mrengo uwe na haki ya kutangaza wagombea ishirini na tano tu (25). Hatua hii itapunguza upotevu wa rasilimali na kurahisisha wananchi kuchagua mgombea anayefaa.

Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid ash-Shuhada aliendelea: kuzungumzia uchaguzi si kwa maana ya kutoka katika ngazi ya muqawama, bali ni mtiririko wa muqawama mwingine wenye masharti, changamoto na mbinu zake maalumu — muqawama huu haukuwa mdogo kwa umuhimu kuliko ule wa awali; bila mfumo huo, kazi inaweza kuwa bila tija, bila matokeo wala lengo.

Alisema: uamuzi wetu wa kushiriki katika uchaguzi wa bunge unatokana na imani hii kwamba; uamuzi huo wa kisiasa ni dhamana kwa ujumbe wa muqawama, kimbilio la silaha zake, utunzaji wa damu za mashahidi wake na kufanikisha malengo yake.

Kwa kumalizia, alisema: Hashd al-Shaabi bado wanangoja kupitishwa rasmi na utekelezaji kamili wa sheria itakayowahakikishia haki za wanajeshi wake; iwapo miongoni mwa wabunge wangekuepo waumini wengi wanaoelewa umuhimu wa Hashd bungeni, sheria hii ingepitishwa bila kizuizi. Uchaguzi unapaswa kuchukuliwa kama mapigano halisi — silaha yake ni kura na uwanja wake ni sanduku la kura — eneo lenye changamoto nyingi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha