Jumapili 26 Oktoba 2025 - 20:24
Njia ya Kukutana na Mtukufu Imam Mahdi (a.s)

Hawza/ Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi ya Mi’raj anatufahamisha kipimo na kigezo ambacho kushikamana nacho kunaweza kuyaangazia macho yetu kuudiriki uzuri wa nuru ya Mtukufu Imam Mahdi (a.s).

Shirika la Habari la Hawza – Qur’ani Tukufu inaitaja radhi ya Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo thawabu ya juu kabisa kwa waumini, kwa kusema:

«وَعَدَ اللَّهُ الْمُؤْمِنِینَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِی مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِینَ فِیهَا وَمَسَاکِنَ طَیِّبَةً فِی جَنَّاتِ عَدْنٍ وَرِضْوَانٌ مِنَ اللَّهِ أَکْبَرُ ذَلِکَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِیمُ.»

“Mwenyezi Mungu amewaahidi waumini wanaume na wanawake bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele; na makazi safi katika bustani za milele. Na radhi ya Mwenyezi Mungu ni bora zaidi. Huo ndio ushindi mkubwa.”  (1)

Sherehe:

Miongoni mwa neema zote za kidunia na za Akhera, kilicho bora zaidi ni daraja la radhi ya Mwenyezi Mungu. Kwa maneno mengine, mtu anayefanya kila jambo kwa lengo la kupata radhi ya Mwenyezi Mungu, kwa hakika amenunua neema zote, uzuri na thawabu za dunia na Akhera.

Lakini ikiwa mtu atfanya mambo yake kwa lengo tofauti na kupata radhi ya Mwenyezi Mungu, hatapata chochote isipokuwa hasara na majuto. Kuna aina tatu za radhi katika maisha ya Mwanadamu: radhi ya nafsi, radhi ya watu, na radhi ya Mungu.

Ndiyo, kutafuta radhi ya nafsi au ya watu si jambo baya iwapo tu jambo hilo litakuwa ndani ya mipaka ya radhi ya Mwenyezi Mungu. Lakini ikiwa matendo ya mtu hayafanywi kwa ajili ya kuipata radhi ya Mwenyezi Mungu, basi mtu huyo atakuwa ni mwenye kupata hasarahapa duniani na kesho akhera.

Mtu mmoja kutoka Kufa alimuandika barua Imam Hussein (a.s) akimuuliza: “Ni ipi kheri ya dunia na Akhera?”

Imam (a.s), baada ya kumtukuza Mwenyezi Mungu, alimjibu:

“Mtu Yeyote aitafutaye radhi ya Mungu kwa gharama ya kuwachukiza watu, Mwenyezi Mungu humtosheleza katika mambo ya watu. Na yeyote aitafutaye radhi ya watu kwa kumchukiza Mungu, Mwenyezi Mungu humuachia watu. (2)

"Na kwa hakika, iwapo mtu ataachwa ajitegemee bila msaada, au akajisalimisha kwa watu ambao lengo lao kuu ni kujiridhisha wao wenyewe, basi atakuwa amepoteza kila kitu alichonacho na anachomiliki."

Njia ya Kukutana na Imam wa Zama (a.s)

Katika dua ya Nudba, tunamsemesha Imam Mahdi (a.s) namna hii:

«هَلْ إِلَیْکَ یَابْنَ أَحْمَدَ سَبِیلٌ فَتُلْقی؟»

“Ewe mwana wa Ahmad! Je, kuna njia ya kukutana nawe?”

Ili kupata jibu la swali hili, tunarejea Hadithi ya Mi’raj. Katika sehemu ya hadithi hiyo, Mwenyezi Mungu anataja thawabu ya yule anayefanya jambo kwa ajili ya kuipata radhi yake:

Mwenyezezi Mungu anamsemesha Mtume wake (saww) kwa kusema:

«فَمَنْ عَمِلَ بِرِضَایَ أُلْزِمُهُ ثَلاَثَ خِصَالٍ: ...»

“Yeyote atakayefanya kwa ajili ya kupata radhi yangu, nitamjaalia mambo matatu…”

Jambo la tatu ni:

«مَحَبَّةً لاَ یُؤْثِرُ عَلَی مَحَبَّتِی مَحَبَّةَ اَلْمَخْلُوقِینَ فَإِذَا أَحَبَّنِی أَحْبَبْتُهُ وَ أَفْتَحُ عَیْنَ قَلْبِهِ إِلَی جَلاَلِی وَ لاَ أُخْفِی عَلَیْهِ خَاصَّةَ خَلْقِی.»

“Upendo nitakaompa ambao hautapendelea upendo wa viumbe juu ya upendo Wangu. Atakaponipenda, nami nitampenda, na nitafungua macho ya moyo wake kuelekea utukufu Wangu, wala sitamficha waja Wangu maalumu. (3)

Je, kuna mja maalumu zaidi kuliko Imam Mahdi (a.s) katika zama hizi?

Katika kipindi cha ghaiba ambacho kwa hekima ya Mungu Imam wetu amewekwa nyuma ya pazia, kwa kushikamana na kipimo hiki cha kimungu “Yeyote afanyaye mambo kwa ajili ya kupata radhi Yangu”  tunaweza, - iwapo ni kwa maslahi ya Mungu, - kufuzu na kukutana na mpendwa wetu.

Imeandaliwa na kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Shirika la Habari la Hawza

Rejea:

1- Surat At-Tawba, aya ya 72

۲- قَالَ اَلصَّادِقُ عَلَیْهِ السَّلاَمُ: «أَنَّ رَجُلاً مِنْ أَهْلِ اَلْکُوفَةِ کَتَبَ إِلَی أَبِی اَلْحُسَیْنِ بْنِ عَلِیٍّ عَلَیْهِ السَّلاَمُ یَا سَیِّدِی أَخْبِرْنِی بِخَیْرِ اَلدُّنْیَا وَ اَلْآخِرَةِ فَکَتَبَ صَلَوَاتُ اَللَّهِ عَلَیْهِ بِسْمِ اَللّهِ اَلرَّحْمنِ اَلرَّحِیمِ أَمَّا بَعْدُ فَإِنَّ مَنْ طَلَبَ رِضَا اَللَّهِ بِسَخَطِ اَلنَّاسِ کَفَاهُ اَللَّهُ أُمُورَ اَلنَّاسِ وَ مَنْ طَلَبَ رِضَا اَلنَّاسِ بِسَخَطِ اَللَّهِ وَکَلَهُ اَللَّهُ إِلَی اَلنَّاسِ وَ اَلسَّلاَمُ.» 

3- Bihar al-Anwar, juzuu ya 74, uk. 21

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha