Jumatatu 27 Oktoba 2025 - 22:41
Simulizi ya Mama Muirani Alie Sababisha Sauti ya Kujitolea Isikike Ulimwenguni

Hawza/ Fasihi ya kujitolea ya Iran imepiga hatua mpya kuwaelekea hadhira wa kimataifa baada ya kuchapishwa kwa tarjama ya Kituruki cha Istanbul.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, ikinukuu kutoka Idara ya Mahusiano ya Umma ya Umoja wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu, kitabu تب ناتمام“Joto lisiloisha” kilichoandikwa na Zahra Hosseini Mehrabadi kimepokelewa kwa hamasa kubwa na wasomaji wa Uturuki.

Kazi hii, ambayo hivi karibuni imetarjumiwawa na kuchapishwa kwa lugha ya Kituruki cha Istanbul na Maktaba ya Ansuz, ni simulizi halisi na inayogusa moyo kuhusiana na maisha ya Shahla Manzavi, mama wa shujaa aliyepoteza maisha vitani, Hussein Dokhanji.

“Joto lisiloisha”, kwa mtazamo wa kina kuhusu athari endelevu za vita na nafasi ya familia za mashahidi na majeruhi wa vita, imeweza kueleza kwa uwazi wa kipekee taswira ya kibinadamu yenye uchungu, uvumilivu na ujasiri wa mama mmoja wa Kiirani.

Kitabu hiki, sambamba na kuangazia dhana za kujitolea na shahada, kinaonesha namna upendo wa mama unavyoweza kuvuka mipaka ya mataifa na kuwa lugha ya ulimwengu nzima.

Taasisi ya Bayan Goster Fajr katika taarifa yake kutokana na mnasaba wa kuchapishwa kwa tarjuma hii imesema:

“Kitabu Joto lisiloisha, si tu kazi ya kifasihi, bali ni hati yenye thamani ya mapambano na ustahimilivu wa wanawake wa Kiirani, waliotengeneza ujasiri na utukufu chini ya kivuli cha kujitolea. Kazi hii inaweza kuwa chanzo cha hamasa kwa vijana katika kuelewa thamani za kibinadamu na kiroho.”

Kwa kuchapishwa kwa tarjama ya kitabu hiki nchini Uturuki, inatarajiwa kwamba kazi nyingine zenye mada za fasihi ya kujitolea na muqawama pia zitazidi kuwavutia wasomaji wa kimataifa.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha