Jumatatu 20 Oktoba 2025 - 07:51
Kuboresha na kuongeza uwezo wa kuhudumia mazuwari wa Ataba Tukufu

Hawza/ Kwa mujibu wa mipango mipya ya Ataba Tukufu ya Imam Hussein (a.s), eneo la Haram linapanuliwa kwa kuchukua eneo jirani na haram hiyo, hatua ambayo inalenga kuboresha huduma kwa mazuwari wa haram hiyo tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika mpango mpya wa Ataba hiyo, ardhi na eneo lililo jirani na Haram ya Imam Hussein (a.s) limekabidhiwa rasmi kwa kitengo husika ili kuboresha huduma kwa mazuwari, hususan katika kipindi cha Arbaeen, na kutumia vyema miundombinu iliyopo ili iweze kukidhi mahitaji ya idadi kubwa sana ya mazuwari wa Arbaeen ya Imam Hussein (a.s).

Hatua hii ni sehemu ya mfululizo wa mipango iliyowekwa kwa ajili ya kuongeza ubora wa mapokezi na huduma kwa mamilioni ya mazuwari wa Arbaeen ya Imam Hussein (a.s) katika miaka ijayo.

Chanzo: Karbala Now Agency

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha