Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Yasin Musawi, Imamu wa Ijumaa wa Baghdad na mmoja wa walimu mashuhuri wa Hawzah ya Najaf Ashraf, katika khutba za Ijumaa alisisitiza juu ya masuala ya kitaifa na ya kieneo, na kuirejesha mamlaka ya Iraq, msimamo wa umma wa Kiislamu dhidi ya uvamizi wa Ghaza na athari za matukio ya hivi karibuni nchini Qatar, kuwa miongoni mwa vipaumbele muhimu zaidi.
Alianza khutba kwa kukumbusha umuhimu wa kushiriki kwenye uchaguzi, akasema ushiriki kuwa ni jukumu la kitaifa, na akaonya kuwa kususia uchaguzi “kunafungua tena mlango wa kupenya kwa mafisadi,” alisisitiza kuwa kipimo cha kuchagua kinapaswa kuwa ni ustahiki na mipango ya kweli ya wagombea, na siyo kauli za udanganyifu kama “huduma” ambazo kimsingi ni wajibu wa kawaida wa kila serikali na siyo mradi wa kisiasa.
Ayatullah Musawi aliendelea kwa ukali kukosoa “maamuzi ya kisiasa ya Iraq kuwa tegemezi kwa wageni” na kusema: “Mradi wetu mkuu ni uhuru na mamlaka, hakuna serikali itakayokuwa na nguvu endapo itaendelea kubeba masharti ya kigeni, iwe kutoka Marekani au sehemu nyengine.”
Katika sehemu nyingine ya khutba, alitaja matukio ya hivi karibuni nchini Qatar kuwa ni “funzo dhahiri kwa serikali za Ghuba ya Uajemi” ambazo zimejifariji kwa uungaji mkono wa Marekani, na akabainisha: “Suluhisho la kweli liko katika umoja wa serikali, mataifa na nguvu za kieneo, siyo katika kutegemea mgeni ambaye katika nyakati za hatari hajawahi kuwa mdhamini wa usalama na uhuru.”
Imamu wa Ijumaa Baghdad, huku akikosoa kutozaa matunda kwa maazimio ya mikutano ya viongozi wa Kiislamu na Kiarabu, aliitambulisha kuwa ni “wino kwenye karatasi” na akaongeza: muda wa kuwa maazimio hayo hayatafuatiwa na hatua za kivitendo, hayatakuwa na thamani ya kweli, pia alilaani uendelezaji wa mahusiano ya baadhi ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni, na kinyume chake, akasifu msimamo wa wazi wa Uhispania dhidi ya ubeberu, akasema: “Wakati baadhi ya nchi za Ulaya zimechukua hatua kwa uwazi zaidi, ulimwengu wa Kiarabu bado uko katika kusitasita, na kusitasita huku kunazidisha mateso ya taifa la Palestina.”
Katika sehemu nyingine za hotuba yake, aliielezea Ghaza kuwa ni “tatizo kubwa na lenye kuumiza moyo” na huku akilaani kuzingirwa na mabomu yasiyo koma katika eneo hilo, alisema: “Yanayotokea leo ni jinai kubwa; raia wasio na hatia kila siku damu zao zinamwangwa bila sababu, na zaidi ya watu milioni mbili wamesalia kati ya kufa kwa njaa au kufa chini ya vifusi vya mabomu,” pia msimamo wa Marekani wa kuilaumu harakati ya muqawama kama “sababu kuu ya mateso ya raia” aliuita kuwa ni kuhalalisha jinai za wavamizi.
Ayatullah Musawi, huku akilaumu baadhi ya serikali za Kiarabu kutokana na ukimya na kutofanya lolote mbele ya mauaji ya Wapalestina, alisisitiza kuwa: “Ni jambo la aibu kuwa baadhi ya nchi za Kiislamu hata zimesalia nyuma ya msimamo wa wazi wa baadhi ya nchi za Ulaya, leo tunahitaji hatua halisi na ya pamoja ya Kiislamu, siyo matamko yasiyo na athari.”
Imamu wa Ijumaa Baghdad, mwishoni mwa khutba zake, alibainisha kuwa: “Palestina na ulazima wa kufufua mamlaka ya kitaifa ya Iraq lazima viendelee kubakia katika mstari wa mbele na iwe vipaumbele vya umma, kuendelea kwa migawanyiko na utegemezi kutaiweka daima kanda hii mikononi mwa irada ya wageni.”
Maoni yako