Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad al-Qattan, Mwenyekiti wa Jumuiya ya “Qawluna wa al-‘Amal” na mwanachuoni wa Kisunni wa Lebanon, akizungumza katika hafla iliyofanywa na Kamati ya Wanawake ya jumuiya hiyo katika eneo la Bar Elias nchini Lebanon, alisisitiza juu ya umuhimu wa nafasi ya wanawake waumini katika kuunda vizazi vya muqawama, na akasema kuwa:
“Tunahitaji wanawake waumini ambao wataweza kutupatia mifano kama Sheikh Ahmad Yasin, Abdulaziz al-Rantisi na viongozi wote mashahidi wa Palestina, Ghaza, Lebanon, Yemen na kila mahali pengine.”
Sheikh al-Qattan alimtaja adui kuwa ndiye anayehusika na uvamizi wa kimfumo dhidi ya mataifa ya umma huu, na akarejelea shambulio la mabomu lililolenga majengo ya makazi mjini Doha kwa kisingizio cha kuwepo viongozi wa muqawama humo, na akabainisha kuwa hujuma kama hiyo inaweza kurudiwa katika nchi yoyote ya Kiarabu.
Akasema kuwa: “Adui huyu haamini katika utu, na uvamizi wake dhidi ya Lebanon, Yemen, Palestina na Ghaza unaendelea; kwa hivyo tunahitaji umoja wa kweli wa Kiarabu na Kiislamu.”
Mwanachuoni huyo wa Kisunni wa Lebanon alitoa wito wa umoja na mshikikiano kati ya nchi za Kiarabu na Kiislamu katika kukabiliana na adui mwenye jeuri.
Maoni yako