Kwa mujibu wa ripoti ya kikundi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kituo hiki kimetangaza kwamba kuanzia kuanguka kwa serikali iliyopita miezi tisa iliyopita, kumekuwa na “ongezeko lisilo na kifani la ukatili”, na kimeorodhesha mauaji ya watu 10,672, wakiwemo 3,020 waliouawa kwa kunyongwa hadharani.
Kituo hiki kimebainisha kwamba kuanguka kwa taasisi za usalama na kijeshi hakukuleta uthabiti, bali kuliibua ombwe katika kila kipande cha nchi, na hivyo ukatili na mauaji yakawa jambo la kawaida katika mikoa mingi.
Kimeongeza kuwa vitendo vya kikatili vilivyoshuhudiwa nchini Syria “havikuwa vya kibinafsi”, bali vilikuwa vya kimuundo, vikilenga kusambaratisha mshikamano wa kijamii na kuchochea mgawanyiko kati ya Wasyria.
Mauaji ya raia 8,180:
Kwa mujibu wa Kituo cha Uangalizi wa Haki za Binadamu Syria, kati ya waliouawa 10,672, raia walikuwa 8,180, ambapo watoto 438 na wanawake 620 ni miongoni mwao.
Hali ya mauaji haya ilihusisha “risasi za kiholela”, “mazingira yasiyoeleweka”, pamoja na mauaji yaliyofanywa na vikosi vya usalama vya serikali ya Syria, vikosi vya “Jeshi la Kitaifa” vinavyoungwa mkono na Uturuki, Daesh, uvamizi wa Israel, mashambulizi ya mabomu ya Uturuki, mabaki ya vita na mengineyo.
Kituo kimeeleza pia kuwa raia 883 waliuawa na Idara ya Operesheni za Kijeshi, wakiwemo wanaume 801, wanawake 58 na watoto 24. Aidha, wanaume wengine 56 waliteswa hadi kufa katika magereza ya idara hiyo.
Mauaji ya kunyongwa hadharani, miongoni mwa matukio mashuhuri zaidi:
Kwa mujibu wa kituo hiki, ambacho kimeorodhesha matukio 3,020 ya mauaji ya kikatili, kuongezeka kwa mauaji ya kunyongwa hadharani na mauaji kwa misingi ya utambulisho ndicho kipengele mashuhuri zaidi cha kipindi hiki.
Mauaji ya wanajeshi 2,492:
Kulingana na Kituo cha Uangalizi wa Haki za Binadamu Syria, idadi ya wanajeshi waliouawa imefikia 2,492, wakiwemo watumidhi 1,034 wa Idara ya Operesheni za Kijeshi.
Hotuba zenye mifarakano na simulizi potofu
Kituo kimeeleza kwamba hali hii imesambazwa kupitia maneno ya kichochezi yenye mifarakano yaliyohusisha makabila na misimamo ya kisiasa, kama vile madai kwamba Waalawi ni masalia ya utawala wa zamani, Wadrusi ni mamluki, au Wakurdi wanajitenga—jambo limezidisha migawanyiko na kukwamisha mchakato wa haki ya mpito.
Kampeni hizi hazikujikita tu katika kusambaza simulizi potofu, bali pia ziliwalenga wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu na vyombo vya habari huru, kwa kupitia mitandao ya “trolls” wa kielektroniki walimshambulia yeyote aliyefichua makosa au kudai uwajibikaji wa waliohusika.
Maoni yako