Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, barua ya Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza Tukufu ya Qum kwa wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu
Na shikamaneni nyote pamoja na kamba ya Mwenyezi Mungu, wala msifarakiane, Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, mlipokuwa maadui, akazipatanisha nyoyo zenu, kwa neema yake mkawa ndugu
(Aali Imran, 103)
Kwanza kabisa, tunawapongeza nyinyi waheshimiwa na wasomi wa elimu za Manabii, pamoja na wafuasi wote wa dini ya Muhammad (saw), kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume mtukufu wa Uislamu, Muhammad bin Abdullah (saw).
Leo hii sehemu ya mwili wa Uislamu, yaani Palestina iliyodhulumiwa – hasa mji wa Ghaza – iko mikononi mwa wavamizi na wauaji wa utawala katili wa Kizayuni, ikiwa katika mateso na majeraha, watu wasio na hatia na waliokumbwa na njaa huko Ghaza wanachinjwa hadharani mbele ya macho ya dunia, hata katika mistari ya chakula. Ni wajibu na ni jambo lenye staha kwamba wanazuoni wa Kiislamu – hususan katika chuo chenye heshima na historia Al-Azhar, na pia nchi tukufu ya Kiislamu Misri – wapaze sauti zao kwa nguvu.
Mtume mtukufu wa Uislamu (saw) amesema:
“Mtu yeyote akisikia Mwislamu akipiga kelele akiomba msaada: ‘Enyi Waislamu!’ kisha asimjibu, basi huyo si Mwislamu.”
Vilevile, Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) aliwausia wanawe watukufu Hasan na Husayn (a.s.):
“Kuweni maadui wa dhalimu na muwe msaada wa aliye dhulumiwa.”
Kuundwa kwa dola haramu ya Kizayuni kwa mikono ya Uingereza kuliweka jeraha kubwa moyoni mwa Umma wa Kiislamu, na leo hatari yake inahisiwa zaidi kuliko wakati wowote, sera ya Marekani ya kukabidhi eneo la kusini-magharibi mwa Asia mikononi mwa Israel, kwa hakika inamaanisha kuhalalisha jinai za kumwaga damu nchini Syria na kusisitiza mpango wa kuunda “Israel Kubwa.” Hili limethibitisha kuwa Israel na mabwana wake wa kikoloni hawatashindwa kufanya uhalifu wowote dhidi ya Umma wa Kiislamu. Katika hali hii, wanazuoni wa Kiislamu – hasa wanazuoni wa Al-Azhar – wana jukumu la kuamsha Waislamu na kuwasaidia wanyonge wa Ghaza. Ukimya wa wanazuoni wa dini umeusukuma zaidi watawala wa Kiislamu kwenye njia ya kujisalimisha na kupatana kwa maslahi ya Israel na Marekani.
Kundi ovu la Kizayuni likifanikiwa kukandamiza harakati ya kishujaa ya watu wa Ghaza, basi hivi karibuni litayavamia maeneo mengine ya Kiislamu, na kwa mujibu wa Aya Tukufu: Wanawachinja watoto wenu wa kiume na kuwaacha hai wake zenu (Al-Baqara, 49) litaendelea na jinai dhidi ya Umma wa Kiislamu.
Wakati huu ambapo wananchi wa Ulaya, Australia, Marekani na mataifa mengine wameinuka kupinga Israel na jinai za Magharibi huko Ghaza, kimya cha mataifa ya Kiislamu katika baadhi ya nchi hakipaswi kutokana na kutojali kwa baadhi ya wanazuoni wa dini kuhusu msingi wa Uislamu na kutokuwa na masikitiko juu ya dhulma dhidi ya watu wa Palestina.
Leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo ngome kuu ya mapambano dhidi ya ukafiri na uadui wa kidunia, na Mtukufu Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi) ndiye mbebaji bendera wa mapambano haya, vitisho vya rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi wa Iran, kwa hakika, ni vitisho dhidi ya Uislamu wenyewe, ikiwa hatua hazitachukuliwa, basi uwepo wa Uislamu utakuwa hatarini, kwa misingi hiyo, inafaa sana wanazuoni wa Al-Azhar wachukue nafasi ya uongozi kati ya nchi nyingine za Kiislamu na watangaze kwa uthabiti msimamo wa kutetea watu wa Ghaza, huku wakikuza harakati za uamsho wa Umma wa Kiislamu ili kuutekeleza wasia wa Mtume mtukufu wa Uislamu (saw).
Katika siku hizi ambazo zimepewa jina la Wiki ya Umoja kwa ubunifu wa mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (r.a.), ni wajibu kwa Waislamu wote duniani, kwa huruma na mshikikano, kuzilinda nchi za Kiislamu dhidi yenye fitina za kugawanya na njama za maangamizi za maadui. Ni lazima kuyatahadharisha mataifa ya Kiislamu kuhusu hatari ya uenezaji wa ukaliaji wa mabavu na mipango mibaya ya “kuigeuza Ghaza” au “kuigeuza Syria” nchi zao, na kuwahamasisha wajihusishe na jihadi kwa ajili ya kuwaondoa wavamizi, kulinda umoja wa ardhi za Kiislamu, na kuikomboa Quds Tukufu.
Hakika, kuongoza Umma na kuleta mshikamano miongoni mwa Waislamu ni jukumu la Qur’ani lililo juu ya mabega ya wanazuoni wa Kiislamu, umoja ndio mkakati muhimu zaidi wa Qur’ani kwa ajili ya heshima na nguvu za Umma wa Kiislamu na kuusambaza ulimwenguni ustaarabu wa Uislamu wa Muhammad (saw).
Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza Tukufu ya Qum unanyoosha mkono wa urafiki na mshikamano kwa wanazuoni wote wa nchi za Kiislamu – hususan wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar – na unataka kuwepo uhusiano mpana, wenye nguvu na wa kina baina ya wanazuoni wa Qum na Misri, ili kukuza umoja wa kielimu na kuepuka mifarakano mbele ya maadui wa Uislamu. Bila shaka, utekelezaji wa Aya Tukufu:
{Na shikamaneni nyote pamoja na kamba ya Mwenyezi Mungu, wala msifarakiane}
(Aali Imran, 103)
utaokoa mshikamano na nguvu za ulimwengu wa Kiislamu, na kuvunja njama na mipango yote ya kikoloni ya Marekani, Uzayuni na Ulaya katika ardhi na mataifa ya Kiislamu.
Na shikamaneni nyote pamoja na kamba ya Mwenyezi Mungu, wala msifarakiane.
Amesema kweli Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Aliyeadhim.
Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza Tukufu ya Qum
Maoni yako