Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Ayatullah Mahmoud Rajabi, mjumbe wa uongozi wa Bunge la Wataalamu wa Uongozi (Majlis Khobregan Rahbari), Rais wa Taasisi ya Kielimu na Utafiti ya Imam Khomeini (r.a.), na mjumbe wa Jami‘at al-Mudarrisin ya Hawzah ya Qum, uliotolewa kufuatia mpango ovu wa utawala wa kigaidi wa Marekani dhidi ya taifa tukufu na lenye kusimama imara la Lebanon, ni kama ifuatavyo:
Bismillahir Rahmanir Rahim
“Hakika kundi la Mwenyezi Mungu wao ndio wenye kufaulu.”
Utawala wa kigaidi wa Marekani, baada ya kupokea vipigo vingi vyenye kufedhehesha katika miaka ya hivi karibuni, umejitokeza tena na njama hatari hii kwa dhana yake ya kipuuzi, ili kujenga kinga ya usalama kwa mbwa wake mwitu katika ukanda, Kwa kuidhalilisha akili na heshima ya watu mashujaa wa Lebanon, wanakuja na mpango ovu wa kuivua silaha Hizbullah.
Umma wa Kiislamu, hususan watu wa Lebanon na Palestina—Shia, Sunni na Wakristo—wanajua vizuri kuwa Hizbullah ya Lebanon tangu mwanzo wa kuundwa kwake hadi sasa haijawahi kukoma katika juhudi zake kwa ajili ya heshima, hadhi na nguvu ya Umma wa Kiislamu, na hasa kwa ajili ya watu wanyonge na wenye kusimama imara wa Lebanon, kwa kuwa Hizbullah imetokana moja kwa moja na jamii ya Kilebanon na imefanya ukakamavu wake katika kupambana na maadui wa taifa hilo na kulinda heshima na kuinua hadhi ya Lebanon.
Viongozi wa chama hiki kitukufu—kuanzia daraja za juu zaidi ambazo ni mashahidi wakubwa wa Umma wa Kiislamu kama Sayyid Abbas Musawi, Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin (ra) pamoja na mwanachuoni mwema na mpiganaji, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Naeem Qassem (hf)—hadi askari waliotoa maisha yao katika uwanja wa mapambano katika miongo mbalimbali, kwa maneno, vitendo na damu yao wamethibitisha kwamba heshima, hadhi na maslahi ya watu wa Lebanon na Umma wa Kiislamu wameyatanguliza juu ya starehe zao na familia zao.
Hizbullah hii, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu na msaada wa watu wa Lebanon, kupitia vita vitatu vizito—vita vya mwaka 2000, vita vya Tamuz, na mapambano ya Awli-Ba’s—kwa kutoa mashahidi na majeruhi, iliweza kumkimbiza mnyang’anyi huyu muuwaji wa watoto aliyefika hadi Beirut, na ikawarudishia watu wa Lebanon na Umma wa Kiislamu katika Asia Magharibi heshima na nguvu waliokuwa wamezipoteza.
Njama ya kuivua silaha Hizbullah, ambayo ni ndoto ya Marekani na utawala wa Kizayuni, haitatimia kamwe, tishio hili, ambalo linalenga kuirudisha Lebanon katika enzi za fedheha na maangamizi, litageuka, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na kwa ushujaa wa Hizbullah na mitazamo mbalimbali ya mashujaa wa Lebanon, kuwa fursa adhimu kwa Umma wa Kiislamu, hususan watu wa Lebanon na Palestina, na Inshallah litakuwa hatua nyingine kuelekea kufutika na kuangamia kwa utawala wa Kizayuni.
Uhusiano wa Hizbullah na watu wa Lebanon hauwezi kuvunjika. Marekani, utawala wa Kizayuni na vibaraka wao wanaotaka kwa vita vya kisaikolojia kufanikisha malengo ya Kizayuni, ndoto yao hii watazika makaburini, kwani Hizbullah imo ndani ya nyoyo za watu wa Lebanon, watu wa Lebanon bado wanakumbuka vizuri mapokezi waliyoyafanya kwa mashujaa wao waliokuwa washindi katika vita vya siku 33, na wanajivunia hilo.
Watu wa Lebanon na Palestina, pamoja na heshima na hadhi yao, wako katika nyoyo za mashujaa wa Hizbullah, na Hizbullah, kama ilivyokuwa siku za nyuma, katika njia hii ya kulinda malengo na thamani za Kihislamu, kibinadamu, pamoja na wanyonge katika ulimwengu na wanao nyanyaswa, imesimama imara mpaka mwisho wa mauti.
Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya watu mashujaa wa Lebanon waliowalea wanaume mashujaa na wanawake jasiri!
Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya mashahidi wapendwa na majeruhi wenye kusimama imara wa Lebanon waliotengeneza hadithi ya ushindi wa damu juu ya upanga na imani juu ya ukafiri!
Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya familia subira za mashahidi na majeruhi wa heshima wa Lebanon, na salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Hizbullah na wapiganaji wote waaminifu wa Lebanon na Palestina, ambao kwa imani na kutegemea ahadi za Mwenyezi Mungu wanasonga mbele katika njia ya daima ya ushindi wa muqawama.
Naam, hii ndio ahadi ya Mwenyezi Mungu kwamba: “Na kwa yakini Mwenyezi Mungu atamnusuru anaye mnusuru Yeye.”
Maoni yako