Jumatatu 25 Agosti 2025 - 22:46
Jawabu la Amir wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Pakistan kuijibu barua ya Ayatollah A’rafi kuhusiana na Ghaza

Hawza/ Maulana Fazlur Rahman, Amir wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Pakistan, katika barua yake kwa Ayatollah A’rafi, aliusifu msimamo wa Iran kuhusu Ghaza na kusisitiza juu ya umoja wa Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Palestina

Kwa mujibu wa Idara ya Habari za Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, kufuatia barua iliyotumwa kutoka kwa Ayatollah A’rafi kwenda kwa Maulana Fazlur Rahman, Amir wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Pakistan, jibu rasmi na lenye maelezo ya kina kutoka kwake limepokelewa, Katika barua hiyo ambayo imesisitiza mshikamano wa kidini na kibinadamu wa pande mbili kuhusu suala la Palestina, kiongozi mashuhuri wa Kisunni wa Pakistan amesifu msimamo wa maulamaa wa Iran na akatoa wito wa umoja kwa Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wanyonge wa Ghaza.

Matini kamili ya barua hiyo, ambayo inabeba mitazamo ya pamoja na wito wa kushirikiana kwa upana zaidi kimataifa, ni kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Bwana Alireza A’rafi
Mkurugenzi wa Hawza za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

As-salaam alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh

Kwa anuani ya Rais wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Pakistan ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan, ninakushukuru kwa dhati kutokana na barua yako ya kirafiki na kindugu, hisia ulizozieleza wewe katika kuwaunga mkono watu wa Palestina na watu wa Ghaza ni za kusifiwa mno na zinastahiki pongezi.

Sisi tunaamini kwamba suala la Palestina si suala la kisiasa pekee, bali ni suala la kidini, kimaadili na kibinadamu la Umma mzima wa Kiislamu, ili kulitatua, maulamaa, wasomi, vyuo vikuu na harakati za Kiislamu kutoka pande zote za dunia lazima waungane pamoja.

Mafundisho ya Qur’ani Tukufu uliyoyanukuu katika barua yako ni chanzo cha uongofu kwetu sisi sote, tunafurahi kwamba msimamo uliochukuliwa na uongozi wa kielimu na kidini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika jambo hili unalingana na matakwa ya haki, uhuru na heshima ya binadamu.

Sisi tunaunga mkono kikamilifu wito wako wa kusonga mbele katika mapambano ya kuwatetea wanyonge wa Ghaza katika ngazi ya kimataifa, na tunakuhakikishia kwamba hatutaacha kushirikiana kwa namna yoyote ile.

Kwa muktadha huu, tunatoa wito pia kwa nchi za Kiislamu kote duniani, taasisi za kielimu na kiakili za kimataifa, na pia kwa mataifa yote yanayopenda uhuru, kwamba msaada wa vitendo na msaada wa kimaadili kwa ajili ya kukomesha kuzingirwa watu wa Ghaza ni jukumu lao la kidini na kibinadamu.

Mahitaji ya wakati huu ni kwamba Umma wa Kiislamu, kwa mshikamano na mshikikano wao wa ndani, wapaze sauti zao dhidi ya dhulma hii ili mapambano ya ukombozi wa Qibla ya Kwanza yaweze kufanikishwa.

Na Mola Mtukufu atupe tawfiki ya kuchukua nafasi yenye taathira katika kutetea haki, kuwaunga mkono wanyonge na kudumisha umoja kwa Umma wa Kiislamu. Aamin.

Wassalaam alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh

Mnyenyekevu wako,
Fazlur Rahman
Amir wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Pakistan

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha