Jumapili 24 Agosti 2025 - 00:53
Imam ni kioo cha rehema isiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu

Hawza/ Imam zaman (as) ingawa yupo kwenye ghaiba, lakini ni wingu la rehema linaloendelea kunyesha daima na kulipa uhai na bashasha jangwa kavu la watu, na ni mwenye kunyimika yule ambaye hatanusa ladha ya mapenzi kutoka kwenye chemchemi hii ya huruma, na asihisi upendo huu

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Moja ya pembe zisizojulikana za Imam Asr (as) ni mapenzi na huruma yake kwa wanadamu, cha kusikitisha ni kwamba tangia zama za kale imekuwa hivyo kwamba Imam ametambuliwa tu kwa upanga, umwagaji damu, ghadhabu na kulipa kisasi, na kuoneshwa kwa sura ya ukali na ukatili, hali kadhalika, wakati ambapo yeye ni kioo cha rehema isiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu, baba mwenye huruma wa umma, rafiki mwaminifu na mwenza mwenye nia njema.

Katika hadithi ya Qudsi, mwishoni mwa kutajwa Maimamu watoharifu as imekuja:

وَأُکملُ ذَلِکَ بِابْنِهِ م‏حمد رَحْمَةً لِلْعَالَمِین‏

“Na nitakamilisha \[mlolongo wa Maimamu] kwa mwanawe Muhamad hali ya kuwa ni rehema kwa walimwengu wote.”
(Kāfī, juz. 1, uk. 528)

Na katika kauli iliyopokelewa kutoka kwake mwenyewe inasema:

أَنَّ رَحْمَةَ رَبِّکُمْ وَسِعَتْ کُلَّ شَی‏ءٍ وَ أَنَا تِلْکَ الرَّحْمَة

“Hakika rehema ya Mola wenu imeshughulikia kila kitu, nami ndiye rehema hiyo isiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu.”
(Bihār al-Anwār, juz. 53, uk. 11)

Na katika kauli ya Maimamu watoharifu as imeelezwa hivi:

وَ أَشْفَقَ عَلَیهِمْ مِنْ آبَائِهِمْ وَ أُمَّهَاتِهِم‏

“[Imam] ana huruma zaidi kwa watu kuliko baba zao na mama zao".
(Bihār al-Anwār, juz. 25, uk. 117)

Imam wa zama (as) ni mlezi mkuu na mwalimu mwenye huruma kwa wanadamu, na ni baba mwenye upendo kwa watu, daima na kila wakati anazingatia kheri na maslahi yao, na pamoja na kutokuwa na haja nao, huwanyeshea wingi wa fadhila na ihsani, kama alivyosema mwenyewe:

لَوْ لَا مَا عِنْدَنَا مِنْ مَحَبَّةِ صَلَاحِکُمْ وَرَحْمَتِکُمْ وَالْإِشْفَاقِ عَلَیکُمْ لَکُنَّا عَنْ مُخَاطَبَتِکُمْ فِی شُغُل

“Kama isingelikuwa kwamba tuna mapenzi ya kuwatakia uboreshaji wa mambo yenu, na tunawaangalia kwa rehema na huruma, tungelikuwa tumejishughulisha mbali na kuzungumza nanyi”
(Bihār al-Anwār, juz. 53, uk. 179)

Kwa hiyo, Imam wa zama (as) ingawa yupo ghaiba, lakini ni wingu la rehema linaloendelea kunyesha daima na kulipa uhai na bashasha jangwa kavu la watu, na ni mwenye kunyimika yule ambaye hatanusa ladha ya mapenzi kutoka kwenye chemchemi hii ya huruma, na asihisi upendo huu.

اللهم هَبْ لَنَا رَأْفَتَهُ وَرَحْمَتَهُ وَدُعَاءَهُ وَخَیرَه

“Ewe Mwenyezi Mungu! Tunusurishe kwa upole wake, rehema yake, dua yake na wema wake.”
(Mafātīḥ al-Jinān, Du‘ā’ Nudbah)

Utafiti huu unaendelea...

Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho “Negin-e Āfarinish” huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha