Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kugawa tabarruk za Imam Husein (a.s.) imefanyika kwa ushirikiano wa wanazuoni wa Kishia na Kisunni katika mji wa Khulna, katika hafla hiyo, wanazuoni mashuhuri wa Kisunni kutoka jumuiya ya “Jamiat Muhibbin Ahlul-Bayt (a.s.)” pia walihudhuria na kushiriki bega kwa bega na wanazuoni wa Kishia katika ugawaji huo.
Lengo la tukio hili si tu kumuenzi Imam Husein (a.s.) na kuonesha mapenzi kwake, bali pia ni alama ya wazi ya mshikamano, udugu na maelewano miongoni mwa Waislamu, tukio hili linaashiria mshikikano madhubuti kati ya Shia na Sunni na jitihada za kuimarisha mshikamano wa kidini katika jamii.
Washiriki wa hafla hiyo walipokuwa wakirejelea ujumbe wa Ashura, walisisitiza kwamba: “Funzo kubwa la Karbala ni kujitolea kwa ajili ya haki, uadilifu na ubinadamu,” Fikra za Imam Husein (a.s.) si mali ya Mashia pekee, bali ni chanzo cha msukumo na hamasa kwa Uislamu mzima, ndiyo maana Arubaini katika zama hizi imekuwa alama ya mshikamano na maelewano kwa Waislamu duniani kote.
Hafla kama hizi zinazofanyika Khulna, mbali na kuimarisha mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s.), pia zinaweza kuwa na nafasi muhimu katika kukuza amani, kuhimiza kuishi kwa maelewano na kuimarisha mshikamano wa kidini nchini.
Maoni yako