Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya tamko la Kituo cha Usimamizi wa Hawza katika kuthamini mahudhurio ya watu kwenye maadhimisho ya Arubaini na ukarimu wa serikali pamoja taifa la Iraq, ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
“Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.
” (Al-Hajj, 32)
Mjumuiko mkubwa wa Arubaini ya Husein (a.s.) mwaka huu, kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita, umekuwa ni kielelezo cha kutukuza alama za Mwenyezi Mungu na Uislamu, kwani Husein bin Ali (a.s.) huko Karbala alidhihirisha kwa damu yake mwenyewe, na damu za watoto wake pamoja na maswahaba wake, sura kuu ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na akawa mfano mkuu wa utiifu kwake, tukio hili adimu la kimataifa limeuonesha ulimwengu upeo mpana wa Ashur'a na kuwa alama ya mshikamano kwa Umma wa Kiislamu na mapenzi yao kwa thamani za kimungu.
Na bila shaka mwaka huu, adhama ya mahudhurio haya imeambatana na hamasa na sauti za kusimama dhidi ya kina Yaziyadi wa zama hizi; wale ambao leo hii wanawauwa kwa mabomu na makombora watu wanyonge wa Ghazza, wakiwatesa kwa njaa na kiu, na kuvunja mipaka yote ya utu, Arubaini ya mwaka huu pia imekuwa ni jukwaa la mshikamano wa mazuwari kutoka mataifa mbalimbali na taifa la Iran, taifa ambalo limeandika historia na kupewa sifa ya kuwa ngano ya mapambano dhidi ya Shetani wa zama hizi.
Kituo cha Usimamizi wa Hawza, sambamba na kuthamini mahudhurio ya mamilioni ya watu jasiri kutoka Iran na mataifa mengine, na kwa kutoa shukrani kwa wananchi wote na viongozi waheshimiwa walioliwezesha tukio hili kubwa la kibinadamu, kimungu na kistaarabu, na kwa kuishukuru serikali na taifa adhimu la Iraq kwa kuandaa kwa ukarimu na bora mjumuiko huu mkubwa, kinawataka wapenda uhuru wote duniani kuitumia kauli mbiu ya Imam Husein (a.s.) isemayo: “هَیهَاتَ مِنَّا الذِّلَّة – Haitowezekana kwetu kukubali udhalili” kuwa dira yao, wasimame imara dhidi ya ueneaji wa kibeberu, ubaguzi wa kikabila, na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni na waungaji mkono wao, na kuifikisha ulimwenguni kote sauti ya ukweli na uadilifu.
Kituo cha Usimamizi wa Hawza za Kitaaluma
Maoni yako