Kwa mujibu wa shirika la habari Hawza, Jumuiya ya Wawakilishi wa Wanafunzi na Wanazuoni wa Hawza, katika kuwatetea watoto wanyonge wa Ghaza, imetoa tamko lifuatalo:
Bismillahir Rahmanir Rahim
إنا لله وإنا إلیه راجعون
قال الله الحکیم:
بِأَیِّ ذَنبٍ قُتِلَت
Mataifa ya Kiislamu yameifanya siku ya kwanza ya mwezi wa Swafar kama siku ya kufunga kwa ajili ya kuonyesha mshikamano wao na watoto wa Ghaza, tunatarajia kwamba hatua za haraka zitachukuliwa ili kuzuia ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu isishuke juu ya dunia na kwa wanadamu wote, Jamii ya kibinadamu inapaswa kwa kutangaza kuchukia na kuomboleza kwa umma dhidi ya taifa ovu la Kizayuni, hawa wanyama walioshushwa daraja na wasio na sifa za kibinadamu, kujiepusha nao, sauti ya dunia na azma ya ubinadamu lazima ipige kelele dhidi ya matendo ya kishetani yanayofanywa na kundi la Kizayuni, lazima kutoka katika minara ya misikiti na kengele za makanisa, zitoke sauti za huzuni, majonzi na ghadhabu.
Ewe dunia! Unaona tanuri za mauaji ya watoto na umefumba macho na masikio na kufumba midomo yako. "Enyi watu wa dunia"! Vipi mmelala katika usingizi wa ghafla na ili hali hadi wanyama wametangulia mbele yenu kwa hisia na huruma? Amkeni, nakuapieni kwa haki ya ubinadamu, amkeni! Kimya chenu kinatia makali upanga wa wauaji wa Kizayuni, na koo zaidi za watoto zinachinjwa, na katika njia za magofu ya Ghaza damu zaidi inamwagika.
Kutazama na kunyamaza kwenu kumehalalisha kasi na nguvu ya mashine ya vita na wauaji wa watoto, hawa mabwana wachinjaji wa kimataifa, na hili ndilo linalowapa ujasiri wa kuendelea na mauaji haya ya kikatili Palestina.
Bila shaka, wajibu wa kimataifa ni kuchukua hatua za haraka, na dunia inapaswa kuchukua msimamo dhidi ya shetani wa kabila ovu na lenye kiu ya damu kama kundi la muuaji na katili Netanyahu.
Ni dharura ya lazima kwamba haraka iwezekanavyo, Wayahudi ulimwenguni waonyeshe kujiepusha kwao na serikali ya Israeli, hawa wadanganyifu waovu.
Na Wakristo, kwa dakika moja tu, dakika moja pekee, kwa heshima ya watoto waliouawa Ghaza, wapige kengele katika makanisa, na Mheshimiwa Papa, kwa muda wa sekunde moja tu na mara moja tu, kwa heshima ya damu iliyomwagika, atoe amri ya kimya.
Ndiyo, leo:
Silaha chafu zaidi wanayotumia wazayuni wa Israili wanyang’anyi ni kuwaacha watoto wa Gaza wakifa njaa, ili kuwashinikiza Wapalestina na kufaidika kijeshi kutokana na hatua hii.
Lazima kusimama imara dhidi ya hila hizi za kishetani za Israili.
Inapendekezwa kwa Waislamu wote ulimwenguni wafunge siku ya kwanza ya mwezi wa Safar, na kitendo hiki kitangazwe kama “funga ya Umma wa Kiislamu kwa mshikamano wa kiutendaji na watoto wenye njaa wa Gaza”, na madhehebu yote ya Kiislamu, kama umma mmoja wa Qur’ani, kwa njia hii wachochee hisia za kibinadamu ulimwenguni.
Sisi wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi, kwa kupata ruhusa na idhini kutoka kwa wakubwa, na kwa kuomba msaada kutoka kwa wizara ya mambo ya nje, tunataka [(meli za uokozi za Nuhu)] ambazo zitajaa msaada wa chakula kutoka kwa watu, zielekezwe Ghaza, na zitengeneze mazingira ya uwepo wa Jumuiya ya Wawakilishi wa Wanafunzi kwa kutumia meli hizi za kubeba chakula.
Nakuapieni kwa haki ya ubinadamu na heshima, amkeni! Msije mkakaa kimya, kimya chenu kitakifanya kisu cha wauaji wa watoto wa Kizayuni kuwa kikali zaidi na kuchinja koo zaidi za watoto wenye kiu na njaa.
Sasa ambapo mashirika makubwa yenye majina makubwa yamechagua ukimya wa maana, "enyi mataifa"! Sasa basi fanyeni haraka na anzisheni harakati za kiraia za kimataifa kwa ajili ya kuzuia.
"Enyi watawala dhaifu na walioshikwa na tamaa ya madaraka!" Ziepusheni nafsi zenu kuwa vinyago vya Mayahudi wa Israili, na jueni kwamba uzembe huu umeifanya ardhi ya Ghaza kuwa mahali pa kuchinjwa watoto wanyonge na wasio na ulinzi wa Kipalestina.
Mwisho wa ujumbe.
Maoni yako