Jumatano 23 Julai 2025 - 00:23
Katika kati ya moto na njaa, tumaini la Ghaza limeelekezwa kuuelekea Umma wa Kiislamu / Hatua ya haraka kwa Umma wa Kiislamu na taasisi za kimataifa kuvunja kuzingirwa na kufikishwa misaada ya dharura

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani, katika barua mbalimbali amewaomba maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu wamkabili twaghuti wa dhulma, walie njaa ya wanyonge, wapaze sauti zao dhidi ya tawala za Kiislamu, na watake hatua ya haraka kutoka kwa Umma wa Kiislamu na taasisi za kimataifa ili kuvunja kuzingirwa na kufikisha misaada ya dharura na ya kiutu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah A’rafi katika barua kuwaelekea baadhi ya maulamaa na shakhsia kubwa za Kiislamu ameandika kuwa: Kwa moyo uliojaa huzuni kwa sababu ya uhalifu wa kivita wa Wazayuni, na kwa roho iliyojaa udugu wa Kiislamu, ninawasilisha barua hii.

Mkurugenzi wa Vyuo Vikuu vya Dini Irani alisema: Katikati ya moto na njaa, jicho la matumaini la ndugu na dada zetu wa Ghaza limeelekezwa kuuelekea Umma wa Kiislamu, na njaa ya mtoto wa Kiislamu haileti tu machozi machoni bali haiachi udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza aliendelea kwa kusema kuwa; dhulma inayoikumba Ghaza si tu mgogoro wa kisiasa, bali ni jaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuthibitisha ukweli wa madai ya umoja na uamsho wa dhamiri.

Ayatollah A’rafi amewaomba maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu wamkabili twaghuti wa dhulma, walie njaa ya wanyonge, wapaze sauti dhidi ya tawala za Kiislamu, na watake hatua za haraka kutoka kwa Umma wa Kiislamu na taasisi za kimataifa ili kuvunja vizuizi na kufikisha misaada ya dharura na ya kiutu.

Mkurugenzi wa Vyuo Vikuu vya Dini, ameutaka Umma wa Kiislamu na dunia nzima kwa ujumla kuchukua hatua za msingi, na ametangaza kuwa vyuo vya kidini viko tayari kwa ajili ya mkutano au semina ya kimataifa kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa kielimu na kiroho wa Umma wa Kiislamu, aidha alisema kuwa: Marjaa wakubwa wa taqlid, vyuo vya kidini, wananchi jasiri wa Iran, na mhimili wa muqawama wanapaza sauti zao kwa nguvu kwa ajili ya kuwaunga mkono wenye njaa na wapiganaji wa jihadi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha