Jumatatu 21 Julai 2025 - 04:51
Hukumu za Kisheria | Kusikia Aya ya Sajda ya wajibu katika Swala

Hawza/ Mtukufu Ayatollah Khamenei amejibu swali la kifiqhi kuhusu wajibu wa mwenyekuswali pindi anaposikia aya ya sajda ya wajib katika swala za faradhi na zile za sunnah.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika dini ya Uislamu, swala ni mojawapo ya nguzo muhimu za ibada, na ina hukumu na vipengele vya kina ambavyo kuzingatia kwake ni jambo la lazima kwa ajili ya usahihi wa swala, miongoni mwa hukumu hizo ni suala la kusikia aya ya sajda ya wajibu wakati wa swala, ambapo huenda baadhi ya watu wakawa na swali juu ya upi wajibu wao katika hali hiyo. Swali hili la kifiqhi linachunguza suala hilo, na Mtukufu Ayatollah Khamenei amelijibu swali hili, nalo linawasilishwa kwa heshima mbele yenu nyinyi wapendwa.

Swali:

Ikiwa mtu katika wakati wa kutekeleza swala ya faradhi au sunnah atasikia aya ya sajda ya wajib, wajibu wake ni upi? Je, sajda ya swala inachukua nafasi ya sajda ya wajib?

Jawabu:

Katika swala ya faradhi, mtu anaposikia aya ya sajda ya wajib, inampasa kuashiria kwa sajda na kuendelea na swala yake (sajda ya swala haichukui nafasi ya sajda ya wajib).

Katika swala ya sunnah, anaposikia aya ya sajda ya wajib, basi atafanya sajda hiyo kwa namna ya kawaida kisha aendelee na swala, Swala katika hali zote mbili ni sahihi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha