Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mahmoud al-Muwalidi, Mwenyekiti wa Kamati ya Misingi ya Chama cha Ukombozi wa taifa la Syria, alitoa tuhuma za moja kwa moja dhidi ya mfumo wa sasa wa Syria na kuuelezea kuwa ni "nakala iliyofugwa" inayofanya kazi chini ya amri ya Wamarekani na Wazayuni.
Al-Muwaldi alisema kwamba: Mwelekeo wa kiuchokozi ambao makundi yanayojulikana kwa jina la al-Joulani yameuchukua dhidi ya madhehebu mbalimbali ya Kisyria hasa Waalawi, Wakristo na Wadrusi, si chochote ila ni mradi wa kigeni wa kuligawa taifa kwa misingi ya kidhehebu na kimadhehebu.
Maoni yako