Ijumaa 18 Julai 2025 - 08:32
Hakujakuwa na makubaliano wala mazungumzo yoyote na magenge ya kihalifu huko Sweida

Hawza/ Sheikh Hikmat Al-Hijri amekanusha vikali uwepo wowote wa makubaliano, mazungumzo au ruhusa yoyote na makundi ya kihalifu kuhusiana na hali ya mkoa wa Sweida.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Hikmat Al-Hijri, kiongozi wa jamii ya Wadrusi Syria, amekanusha kwa msisitizo uwepo wowote wa makubaliano, mazungumzo au ruhusa kati yake na makundi ya kihalifu kuhusiana na hali ya mkoa wa Sweida.

Sheikh Al-Hijri katika tamko lake amethibitisha kuwa mtu yeyote au taasisi yeyote itakayokengeuka kuachana na msimamo wa pamoja na kuanzisha mawasiliano na makundi hayo au kuunga mkono upande wao, pasi na kujali lolote, itajikuta katika hali ya kuadhibiwa.

Amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kushikamana na msimamo wa pamoja unaoakisi matakwa ya watu wa Sweida na kujitolea kwao kwa ajili ya usalama na uthabiti wa mkoa huo.

Inafaa kutajwa kuwa kile kinachoitwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Syria, baada ya kuongezeka kwa matukio ya kiusalama katika mkoa wa Sweida katika siku chache zilizopita, ilitangaza kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano yamefikiwa katika mkoa huo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha