Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Mirza Jawad Agha Tahrani (ra) katika moja ya kumbukumbu zake anasema: Katika kipindi cha masomo katika Hawza ya kielimu ya Qom, wakati mwingine baadhi ya marafiki wa Haj Agha Ruhullah [Imam Khomeini] walikuwa wakimsisitizia sana ili siku moja ya mapumziko waende matembezini nje ya mji ili apate kupumzika kidogo.
Lakini Agha [Imam] hakuwa anakubali, na nyakati ambapo msisitizo ulikuwa mkubwa mno, alikuwa anakubali kuja lakini kwa masharti mawili:
1. Popote ambapo muda wa swala ungewadia, hata kama ni mahali pasipofaa, swala iswaliwe kwa wakati wake wa mwanzo.
2. Kusiwepo mtu yeyote atakayezungumza jambo ambalo harufu ya kusengenya inaweza kunukia kutoka ndani yake.
Maoni yako