Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Afghanistan limetoa taarifa kuhusu tishio la kuuawa kwa Ayatollah al-Udhma Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu:
{وَلَن تَرضَىٰ عَنكَ ٱلیهُودُ وَلَا ٱلنَّصَـٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهم.}
“Wala hawataridhika nawe Mayahudi wala Manaswara, mpaka uifuate mila yao.” [Al-Baqarah: 120]
Wakati ambapo uvamizi wa kinyama unaofanywa na utawala wa Kizayuni unaoungwa mkono na Marekani dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unaendelea, kwa mujibu wa ripoti za baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi, Rais wa Marekani mwenye tabia za hovyo na Waziri Mkuu muuaji wa watoto wa utawala wa Kizayuni, wametoa vitisho vya kumuua Ayatollah al-Udhma Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ingawa yeye (kama alivyosema mara nyingi) anakaribisha shahada, lakini kutoa tishio dhidi ya kiongozi wa kidini na kiroho wa dini na taifa fulani ni kinyume na mila zote za kimataifa na sheria za kimataifa; jambo ambalo, kwa kuwa ni tendo la kijinga na la kipuuzi, linaweza kuwa na athari hatarishi za kikanda na kimataifa.
Hivyo basi, Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Afghanistan linalaani na kulaani tena vikali kitendo hiki cha kishetani, na linatumia fursa hii kwa mara nyingine tena kuziomba taasisi za Umoja wa Mataifa, hasa nchi za Kiislamu, kuzuia kuendelea kwa uvamizi dhidi ya taifa la Kiislamu la Iran, na kujitahidi katika kuleta amani ya haki.
Wasalamu Alaykum wa Rahmatullah
Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Afghanistan
Maoni yako