Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujatul-islam Mahmoud Muhamadi Araki, msimamizi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa mapinduzi Qum, amesema; Tukio hili lilikuwa ni zingatio la Kimungu na wendawazimu wa adui wa Kizayuni ni sababu tu, Imaam Maasum anasema; Mwenyezi Mungu amewafaradhisha maadui zetu kuwa ni wendawazimu.
Aliendelea kusema: Vikosi va jeshi, Basiji Pamoja na watu wote walikuwa wanatamani wapigane na adui asilia na kwa sasa wendawazimu wa Wazayuni umeweza kuyahakikisha matarajio haya, ambayo ni kupigagana na adui wa asili ambae ni Marekani na Israil, kwa hakika sisi sio tulio anzisha vita hivi, na Mwenyezimungu jambo hili amelihakikisha kutokana na wazimu wa adui.
Yeye aliongeza kusema; Tunamshukuru Mola kwa baraka ya Amiril-muuminin (as) na masiku haya ya Ghadir, vikosi vya jeshi la Irani vitaitumia vyema fursa hii na taufiki ipo pamoja nao, na matarajio yote ya adui yatakuwa ni sawa ana yenye kwenda na maji.
Hujjatlu-islami Muhamadii Arak, mwisho alisema kwamba; Nafikiri ni kweli kwamba vita hivi vimetupatia hasara , lakini kwa msaada wa Mwenyezi Mungu ushindi upo upande wetu, yatupasa kuitumia vyema nafasi hii ili matarajio ya ndani ya nyoyo zetu yaweze kutimia, na matarajio hayo si mengine bali ni kuuangamiza moja kwa moja utawala wa Wazayuni.
Maoni yako