Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah al-Udhma Makarim Shirazi, katika hafla ya kuwavalisha rasmi mavazi ya kidini kundi la wanafunzi wa Hawza ya Qom iliyofanyika katika ofisi yake kwa mnasaba wa sikukuu tukufu ya Ghadir, alirejea kwenye aya ya 67 ya Surah al-Ma’ida (Aya ya Tabligh) ili kufafanua umuhimu wa suala la Uimamu katika Qur’ani Tukufu. Alisisitiza kuwa: Qur’ani Tukufu imetoa ishara mbalimbali kuhusiana na suala la Uimamu, na aya hii tukufu ni miongoni mwa aya ya wazi zaidi na isiyo na mfano wake.
Akinukuu aya isemayo:
«يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ...»
alieleza kuwa aya hii ina mambo matatu muhimu: Kwanza, Mtume Mtukufu (saww) amepewa amri ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu tena kwa msisitizo mkubwa.
Pili, kuacha kufikisha ujumbe huo kumewekwa kuwa ni sawa na kuacha ujumbe mzima wa risala.
Tatu, Mwenyezi Mungu amemuahidi Mtume msaada na ulinzi dhidi ya hatari zinazoweza kumkumba.
Katika kuendeleza mazungumzo yake, aliongeza kuwa: Kwa mujibu wa baadhi ya tafsiri za Ahl al-Sunna, aya hii imehusishwa na hukumu za nyama halali na haramu, lakini kufikisha hukumu hizo hakuhitaji onyo lenye uzito kama hili ambalo linaambatana na ahadi ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume. Kwa hiyo, maana ya aya hii haiwezi kuwa kitu kingine isipokuwa suala muhimu na nyeti kama la Uimamu.
Akinukuu yaliyotajwa katika Tafsiri ya Amthal, alisisitiza: Aya hii haiwezi kueleweka ila kwa tafsiri ya wilaya, na ndiyo ushahidi wa wazi zaidi wa Qur’ani kuhusu Uimamu na uongozi wa Mtume Mtukufu (saww).
Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, huku akiwapongeza wanafunzi waliovaa rasmi vazi la kidini kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadir, alisema: Vazi la ualimwengu ni vazi la askari wa Imam wa Zama (aj), na anayelivaa anakuwa ameingia katika hatua mpya ya maisha, hatua ambayo imejaa majukumu mapya. Lazima mjitahidi kudhihirisha haiba yenu mpya kwa kauli na matendo.
Maoni yako