Jumapili 1 Juni 2025 - 21:41
Takriban Wahubiri 15 elfu watajishughulisha na kufanya Tabligh katika masiku ya Arubaini ya Mwaka Huu

Hujjatul-Islam Murtaza Isteqamat ametangaza kwamba: Mwaka huu, uwepo wa walinganizi katika kipindi cha Arubaini umekuwa na ongezeko kubwa; mwaka uliopita, takriban watu 11 elfu hadi 12 elfu wakiwemo wahubiri wa kiume na wa kike walishiriki katika shughuli hii, na mwaka huu idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia watu 14 elfu hadi 15 elfu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Murtaza Isteqamat, ambaye ni mkuu wa Kamati ya Tabl'igh na Swala wa Makao Makuu ya Kitaifa ya Arubaini, alasiri ya siku ya Jumamosi, katika kikao na waandishi wa habari, alieleza mikakati ya tablighi ya Arubaini ya mwaka 1403 Hijria Shamsiya, na kutangaza kuwa kaulimbiu kuu ya mwaka huu ni "kuzingatia dhana ya kudai haki, kukabiliana na ukiritimba, na kusimama pamoja na wanyonge".

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha