Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Khabar wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Reza Rustami, mkuu wa Kituo cha Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii cha Hawza, katika kikao cha mashauriano kilichofanyika kwa anuani ya "Mahitaji ya Ujumbe wa Kimataifa katika Arobaini", kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ayatollah Haeri (ra) katika kituo cha usimamizi wa hawza, ametangaza utayari wa Kituo cha Vyombo vya Habari cha Hawza kutoa mafunzo ya vyombo vya habari kwa wahubiri wa Arubaini na kufanikisha ufanisi mpana kwenye tukio hili kubwa.
Mkuu wa Kituo cha Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii cha Hawza, akisisitiza juu ya umuhimu wa kuratibu shughuli za vyombo vya habari katika kipindi cha Arobaini, alipendekeza kwamba, kwa kuzingatia uwepo wa wahubiri wengi nchini Iraq na kutokuwepo uwezekano wa guvu kazi, mafunzo yanayohitajika yatolewe kwa wanaojitolea na watu waliotajwa na Idara ya Mahusiano ya Kimataifa kabla ya siku za Arobaini.
Akaongeza: Tuko tayari pia kuweka vifaa vinavyohitajika mikononi mwa watu hawa, ili badala ya kuwa na idadi ndogo ya wanahabari wachache na watengenezaji wa filamu za makala, tuwe na idadi kubwa zaidi ya wanahabari waliopata mafunzo. Wanahabari hawa wanaweza, katika kipindi kifupi, kupata mafunzo ya awali na kutoa nguvu kubwa kwa habari na kusaidia vyombo vya habari katika maudhui.
Mkuu wa Kituo cha Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii cha Hawza, akihitimisha kwa kurejelea uzoefu wa mwaka uliopita, alisema: Mwaka uliopita, kwa mara ya kwanza, ushirikiano wa dhati ulifanyika kati ya Kituo cha Vyombo vya Habari na Idara ya Mahusiano ya Kimataifa katika kufanikisha habari na kurekodi kazi za wahubiri katika kipindi cha Arobaini. Alhamdulillah, filamu mbili za makala zilitengenezwa kuhusu uwepo wa wahubiri katika Arobaini, na tunatarajia idadi hii itaongezeka katika siku zijazo.
Maoni yako