Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika masiku yaliyopita, tovuti ya Kiebrania "Hidabrut" ilitangaza kuwa kampuni ya chakula ya "Nestlé" imeidhinisha ongezeko kubwa la bei katika makumi ya bidhaa zake.
Ongezeko hili la bei ni matokeo ya moja kwa moja ya vizuizi vya baharini vilivyofanywa na Yemen katika Bahari Nyekundu na hivi karibuni pia katika Bahari ya Mediteranea, hasa kwa kuzuia bandari ya kimkakati ya "Haifa" ya Israeli.
Katika mahojiano na "Al-Masirah", wataalamu wawili wa uchumi wamethibitisha kuwa vizuizi vilivyowekwa na Yemen vimelenga sekta kuu za uchumi wa Israeli, na athari zake za moja kwa moja zinaonekana katika maisha ya kila siku ya walowezi katika ardhi zilizokaliwa kimabavu.
"Salim Al-Jadi", mtaalamu na mchumi, katika mahojiano haya alieleza kuwa: Kwa hakika, gharama za malighafi katika uzalishaji zimeongezeka kwa kiwango kikubwa. Gharama za usafirishaji wa malighafi kuelekea Israeli zimepanda kwa zaidi ya asilimia 300.
Akaongeza kwa kusema: Mfumuko huu wa bei unazidi eneo la vyakula na unaathiri pia bidhaa na huduma zinazotolewa kwa walowezi wa ardhi zilizokaliwa kwa mabavu. Israeli inalazimika kuagiza bidhaa zake kupitia njia za mbali zaidi, jambo ambalo linamaanisha kulazimika kutumia fedha nyingi zaidi. Israeli inalazimika kuagiza kupitia njia za ardhini kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, na Jordan, jambo linalozidisha ugumu wa hali na kuongeza gharama kwa mlaji wa Israeli.
"Hassan Sarour", mchumi kutoka Lebanon, alithibitisha tathmini hizi na kusisitiza kuwa usumbufu uliosababishwa na Yemen kwa kufunga mihimili mikuu ya usambazaji katika uchumi wa Israeli, ikiwa ni pamoja na bandari za "El-Rashash" na "Haifa", umeathiri vikali misingi ya utawala huu wa kigaidi.
Akasema: "Tukio hili limewafanya wafuasi wa Israeli kuwa katika hali ngumu zaidi kwani sasa wanalazimika kutumia njia nyengine za anga na bahari. Baada ya operesheni ya Yemen dhidi ya Marekani na Magharibi kufeli kwa mara ya kwanza, Washington yenyewe haiwezi tena kuilinda Israeli. Hii ndio gharama kubwa ambayo Israeli na Marekani wanailipa, na sasa hata washirika wa Israeli wanaona utawala huu kama mzigo wa kiuchumi, kiusalama, na kisiasa."
Inatarajiwa kuwa mfumuko wa bei unaoendelea ndani ya miji iliyokaliwa kwa mabavu utasababisha hali ya kutoridhika kwa wananchi dhidi ya serikali ya Israeli na kusababisha mdororo mkubwa zaidi wa uchumi.
Maoni yako