Jumamosi 24 Mei 2025 - 20:20
Uongo katika Mzaha

Hawza/ Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi amejibu swali lililo angazia kuhusiana na “uongo wa mzaha”.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza - Ayatollah Khamenei amejibu swali linalo angazia kuhusiana na "uongo wa mzaha", ambalo linawasilishwa kwenu kama ifuatavyo.

Hukumu ya Uongo katika hali ya Mzaha

Swali:
Je! Kusema uongo kwa mzaha ni haramu? Kwa mfano, kati ya marafiki tunasemezana kwa mzaha, "kampuni fulani ni yangu" (ingawa si kweli), je, mazungumzo ya aina hii ni dhambi na ni uongo?

Jawabu:
Iwapo lengo la msemaji ni kwamba msikilizaji wa habari hiyo ya uongo aichukulie kwa uzito, basi ni haramu, hata kama sababu ya msemaji kutoa habari hiyo ni kufanya mzaha. Lakini kama msemaji hana lengo hilo na msikilizaji anafahamu kuwa mazungumzo hayo ni mzaha, basi si haramu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha