Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, waandamanaji waliokuwa wakionesha upinzani wao dhidi ya vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel na waliokuwa wakitaka serikali ya Uholanzi isifungamane na utawala huo dhalimu, walikamatwa katika maadhimisho ya Sikukuu ya Uhuru ya Uholanzi.
limeripoti kuwa watu wa Uholanzi walikusanyika kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 80 ya uhuru wa nchi yao baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na baadhi ya waliokuwepo katika hafla hiyo walitoa wito kwa serikali ya Uholanzi kulaani vitendo na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni.
Walipaza sauti huku wakisema: "Si muda ulipita wala sasa – kamwe hatutakubali dhulma kutawala!"
Pia walikuwa na bendera nyekundu ndefu yenye urefu wa mita 80, ambayo waliichukulia kuwa ni ishara ya mstari mwekundu ambao serikali ya Uholanzi inapaswa kuuona kati yake na utawala wa Israel, kwa kuwa watu wa nchi hiyo daima wamekuwa upande wa kupinga dhulma.
Maoni yako