Jumapili 27 Aprili 2025 - 17:15
Ayatollah Arafi: Kanzu Tukufu ya Bwana wa Mashahidi (a.s) ni Ensaiklopidia ya Ustahimilivu

Mudiri wa Hawza nchini Irani katika ujumbe wake kwenye mkutano na wasomi wa mimbari za Kishia alisisitiza kuwa: Kanzu tukufu ya Bwana wa Mashahidi (a.s) ni hati na alama kamili ya damu zilizomwagika kwa ushujaa katika siku ya Ashura kwa ajili ya kumuamini Mola, ustahimilivu katika njia ya haki, uadilifu, na kupinga dhuluma.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa  Shirika la Habari la Hawza, kutoka Karbala al-Mualla, matini kamili ya ujumbe wa Ayatollah Arafi kwenye mkutano wa nne wa kimataifa na wasomi wa mimbari za Kishia na kongamano la kwanza la maombolezo la kimataifa la "Safina al-Najaat" ambalo lilifanyika usiku wa Jumamosi katika Hussainiya ya Wairani wa Azarbaijan huko Karbala, karibu na haram tukufu ya Bwana wa Mashahidi (a.s), ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

"Na tukamkomboa kutokana na kichinjwa adhimu"
"Na hakuna hila wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu Aliye juu na Aliye Mkuu"

Uwepo mtukufu wa Bwana wa Mashahidi, mjukuu wa Mtume Mtukufu wa Uislamu, Imam Hussein (a.s), ni shakhsia ya mbinguni ambayo kutokana na kujitolea na ushujaa, kwa mujibu wa misingi ya Kiislamu na kibinadamu, alisimama imara kupambana na dhuluma na ukandamizaji uliofanuwa na watawala dhalimu wa wakati wake.

Imamu huyo mtukufu katika tukio la kusikitisha la Karbala, daima ameathiri historia ya mwanadamu, na ameonesha kuwa imani, kujitolea, na ushujaa katika kulinda haki na uadilifu ni mambo yenye thamani na ya lazima. Si kwa waislamu wa kishia tu, bali hata wapenda uhuru wa historia wanamtambua Bwana wa Mashahidi (a.s) kuwa ni mfano wa maadili na daraja ya juu kwa wanaotafuta haki duniani, na wanathamini sana kukuza maadili na thamani za kibinadamu ambazo Imam Hussein ametufundisha.

Kutonana muktadha huu, kanzu tukufu ya Bwana wa Mashahidi (a.s) ni hati na alama kamili ya damu zilizomwagika kwa ushujaa katika siku ya Ashura kutokana na imani juu ya Mwenyezi Mungu, ustahimilivu katika njia ya haki, uadilifu, na kupambana na dhuluma. Kujishughulisha na ensaiklopidia hii ya ustahimilivu katika zama hizi ni fursa nzuri ya kuchunguza kwa kina kiutamaduni na kihistoria tukio la Ashura, kwa namna ambayo haitavuruga hata kidogo umoja wa Waislamu duniani, bali itakuwa ni kulipiza haki ya yule aliyedhulumiwa katika historia, na kupitia njia hii, mafundisho na ukweli ambao uhai wa mtukufu huyo ulitolewa kwa ajili yao, yatafikishwa ulimwenguni kote.

Mimi, kwa dhati, nawapongeza na kuwashukuru maulamaa, washairi, waimbaji wa majlisi za maombolezo, waandishi, waimbaji wa mashairi ya kidini, wasanii na wasomi wote ambao kwa kalamu zao, sanaa zao, na maneno yao wamejitahidi kuufikisha ujumbe huu wa uhakika wa Kishia duniani. Pia nawaomba washiriki wote kwenye huu mkutano wa wasomi wa mimbari za Kishia, waliokusanyika kutoka mataifa mbalimbali katika Karbala tukufu, dua njema, na matarajio yangu ni kuwa siku za hivi karibuni, atadhihiri mkombozi wa Ahlul-Bayt (a.s), na hatimae tutakusanyika tena chini ya bendera hiyo hiyo, na kuipeperusha kanzu ya Imam Hussein (a.s). Dhuluma, uonevu, na ukosefu wa haki vitaondolewa duniani kote, na wanyonge wote duniani, hasa watu wa Ghaza waliodhulumiwa, wataonja ladha tamu ya maisha ya Kihusseini.

"Miaka imebadilika maradufu na bado hadithi ya kanzu yako ya kale imesalia thabiti."

Heri kwenu na marejeo mema.

Alireza Arafi
Mkurugenzi(Mudiri) wa Hawza Irani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha