Shirika la Habari la Hawza- Kulingana na mtazamo wa Kishia, Imamu na khalifa wa Mtume huchaguliwa tu kwa amri ya Allah na uteuzi Wake, na Mtume humtambulisha Imamu anaefuata baada yake. Hivyo basi, hakuna mtu wala kikundi chenye haki ya kuliingilia jambo hili.
Udharura wa kuteuliwa Imamu kutoka kwa Allah kuna hoja kadhaa, zikiwemo:
1- Kama Qur’an inavyosema, Mwenyezi Mungu ndiye mtawala wa mwisho wa kila kitu, na wote wanapaswa kumtii Yeye peke yake. Ni wazi kuwa mamlaka hii inaweza kutolewa na Yeye mwenyewe kwa yeyote yule kutokana na ustahiki na maslahi. Kwa hivyo, kama Nabii anavyoteuliwa na Allah, Imamu pia hupata "wilāyah" kwa njia ya uteuzi wa Mungu.
2- Hapo awali tumeeleza sifa za Imamu kama vile "‘ismah" (kuwa maasum) na elimu. Ni wazi kuwa mtu mwenye sifa hizi tena katika kiwango cha juu kabisa hawezi kuchaguliwa isipokuwa na Mwenyezi Mungu, ambaye ni Mjuzi wa yaliyo dhahiri na yaliyo siri kwa wanadamu.
Kama ambavyo Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii Ibrahim (a.s):
"إِنِّی جَاعِلُکَ لِلنَّاسِ إِمَامًا"
Hakika Mimi ninakufanya wewe kuwa Imamu kwa watu." (al-Baqarah: 124)
Kuhusu Nabii Adam (a.s) amesema:
"إِنِّی جَاعِل فِی الأرۡضِ خَلِیفَةً"
"Hakika Mimi nitaweka khalifa katika ardhi." (al-Baqarah: 30)
Kuhusu Nabii Daud (a.s) amesema:
"یَٰدَاوۥدُ إِنَّا جَعَلنکَ خَلِیفَةً فِی ٱلأَرۡضِ فَٱحکُم بَینَ ٱلنَّاسِ بِٱلحَقِّ"
"Ewe Dāwūd! Hakika Sisi tumekufanya khalifa katika ardhi; basi hukumu baina ya watu kwa haki." (Ṣād: 26)
Kuhusu Mtume Muhammad (a.s) amesema:
"یَا أَیُّهَا النَّبِیُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاکَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِیرًا"
"Ewe Nabii! Hakika tumekutuma kuwa shahidi, mbashiri na mwonyaji." (al-Aḥzāb: 45)
Na pia amesema:
"وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً یَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَکَانُوا بِآیَاتِنَا یُوقِنُونَ"
"Na tukajaalia miongoni mwao maimamu waliowaongoza kwa amri Yetu, walipovumilia na wakawa na yakini juu ya Aya Zetu." (as-Sajdah: 24)
Na mengineyo.
Kwa hivyo, kuteua kiongozi, Imamu na kiongozi wa watu ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake.
Imamu al-Ridha (a.s) kuhusu hadhi ya Imamu na sifa zake amesema:
"هَلْ یَعْرِفُونَ قَدْرَ الْإِمَامَةِ وَ مَحَلَّهَا مِنَ الْأُمَّةِ فَیَجُوزَ فِیهَا اخْتِیَارُهُمْ إِنَّ الْإِمَامَةَ أَجَلُّ قَدْراً وَ أَعْظَمُ شَأْناً وَ أَعْلَی مَکَاناً وَ أَمْنَعُ جَانِباً وَ أَبْعَدُ غَوْراً مِنْ أَنْ یَبْلُغَهَا النَّاسُ بِعُقُولِهِمْ أَوْ یَنَالُوهَا بِآرَائِهِمْ أَوْ یُقِیمُوا إِمَاماً بِاخْتِیَارِهِمْ"
Je, watu wanajua thamani ya Imāmah na nafasi yake ndani ya Ummah ili watu waweze kumchagua?
Hakika uimamu ni wenye daraja ya juu zaidi, wenye heshima kubwa zaidi, nafasi iliyo tukufu zaidi na iliyo mbali zaidi (kufikiwa) kuliko watu kuweza kuifikia kwa akili zao au kuweza kuifikia kwa maoni yao au kumweka Imamu kwa chaguo lao.
"إِنَّ الْإِمَامَةَ أُسُّ الْإِسْلَامِ النَّامِی وَ فَرْعُهُ السَّامِی بِالْإِمَامِ تَمَامُ الصَّلَاةِ وَ الزَّکَاةِ وَ الصِّیَامِ وَ الْحَجِّ وَ الْجِهَادِ وَ تَوْفِیرُ الْفَیْءِ وَ الصَّدَقَاتِ وَ إِمْضَاءُ الْحُدُودِ وَ الْأَحْکَامِ وَ مَنْعُ الثُّغُورِ وَ الْأَطْرَافِ الْإِمَامُ یُحِلُّ حَلَالَ اللَّهِ وَ یُحَرِّمُ حَرَامَ"
Hakika Uimamu ni msingi wa Uislamu unaokua na ni tawi lake la juu. Kwa Imamu ndiko kunapatikana ukamilifu wa Swalah, Zakāh, Ṣawm, Ḥajj, Jihād, ugawaji wa fa’i na sadaqāt, utekelezaji wa hudūd na ahkām, na ulinzi wa mipaka ya Waislamu.
Imamu ndiye anayehalalisha halali ya Allah, na kuharamisha haramu ya Allah, na kusimamisha mipaka ya Allah, na kuitetea dini ya Allah, na kuwaita watu katika njia ya Mola wao kwa hekima, mawaidha mazuri na hoja zenye nguvu.
"الْإِمَامُ وَاحِدُ دَهْرِهِ لَا یُدَانِیهِ أَحَدٌ وَ لَا یُعَادِلُهُ عَالِمٌ وَ لَا یُوجَدُ مِنْهُ بَدَلٌ وَ لَا لَهُ مِثْلٌ وَ لَا نَظِیرٌ مَخْصُوصٌ بِالْفَضْلِ کُلِّهِ مِنْ غَیْرِ طَلَبٍ مِنْهُ لَهُ وَ لَا اکْتِسَابٍ بَلِ اخْتِصَاصٌ مِنَ الْمُفْضِلِ الْوَهَّابِ فَمَنْ ذَا الَّذِی یَبْلُغُ مَعْرِفَةَ الْإِمَامِ أَوْ یُمْکِنُهُ اخْتِیَارُهُ"
Imamu ni wa kipekee katika zama zake, hakuna anayelingana naye, hakuna ‘ālim anayemfikia, hana mbadala, hana mfano wala mshindani. Ameteuliwa kwa kila fadhila bila kuomba au kujitafutia, bali ni uteuzi kutoka kwa mwenye kufadhilisha, mtoaji. Ni nani basi awezaye kumtambua Imamu au kumchagua?... (Usūl al-Kāfī, j.1, uk.198)
Utafiti huu unaendelea...
Chanzo: Kitabu; "Nengin Afarinesh" pamoja na kufanyiwa marekebisho kiasi.
Maoni yako